14 Maneno ya heshima na umuhimu zake.

Katika kamusi ya karne, kuna maneno muhimu sana mengi inatumika na inahitaji kitabu chenyewe ya kamusi kutafuta maana ya neno hilo. Lakini kila siku kuna maneno muhimu sana kama binadamu na pia watoto wakikuwa ni lazima wajue ili wawe na mahusiliano njema kati na watu kwa maisha ya kila siku na wakati.

food with letters on top on a pink surface
Photo by alleksana on Pexels.com

Kwa kujua maneno ya heshima na kufanya mazoezi kutumia neno hili ni jambo muhimu sana kwa binadamu ila wewe ni mtu mzima au wewe ni mtoto. Hasa kwa watoto maneno hizi ni msingi muhimu wakifunzwa kuwasiliana na Jamii.

Muhimu ya maneno ya heshima.

Muhimu Ya kutumia maneno ya heshima hasa sana kwa watoto ni kuwa:

  • Maneno haya yanatumika kuonyesha kuwa mtoto au mtu mzima ana nidhamu na pia Adabu.
  • Inaonyesha kuwa wewe au mtoto kuwa ana tabia nzuri na heshima.
  • Kutumia maneno hii ina jenga mahusiano na pia urafiki baina ya watu.
  • Inaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye shukrani.
  • Unafunza uwe na heshima kwa wazee na pia mtu yeyote unapatana na yeye.

Je, haya maneno ya heshima ni gani.

Chini yako ni maneno 14 ambao itakufunza na pia ni muhimu sana kama binadamu kuitumia kila siku, na pia kuwafunza watoto kuwa haya maneno ni muhimu sana kuitumikia.

1. Shikamoo.

Ni salamu inatumika kwa kusalimia mtu kwa heshima baina ya watu nae jibu lake itakuwa na jibu lake “marahaba”.

2. Marahaba.

Ni jibu la salamu ya shikamoo. Ikiwa mtu anakusalimu “shikamoo” jibu lako inafaa kuwa “Marahaba”ndio jibu sahihi.

3. Tafadhali.

neno “tafadhali”ni neno inatumika kwa adau ya kuuliza saidizi au kupata lengo fulani kwa kiingereza tunasema “please”.

4. Naomba.

Ni neno la heshima inapotumika watu sana sana wnapotangamana ama kuitaka kitu fulani kwa mfano : Naomba unipe penseli?.

5. Samahani

Samahani ni nrno limetumiks sana ikiwa hujatends mema kwa mtu yeyoye . Kwa leo neno samahani imetumika vizuri vile vile ukipiga simu na mteja hashiki simu, utaskia neno la dada akiongea kwa simu akitumia neno “Samahani”. Pia ni neno muhimi unatumika kuanza kuomba msamaha.

6. Asante

Kwa kiingereza tunasema “Thank you” ni neno instumika kama mtu akikiupa tuzo au zawadi ni vizuri useme “asante”

7. Karibu

neno hili ni jibu la Asante na pia ni neno “Hodi” ikiwa mtu akibisha mlango kwa adabu kabla aingie ofisi la mtu au mahali popote , “Hodi” hutumika na jibu lake sahihi ni “Karibu”.

8. Hodi

Ukifika kwa nyumba la mwenyewe au pia mahali popte unaendapo kuona mtu, Ni vizuri kubisha mlango na kutumia neni hodi kwa kuwa ni neno la heshima. Neno au jibu unafaa kutarajia kwa nwno hodi ni “Karibu.”

9. Pole

Kila mtu katika Dunia hii amefanya makosa. Na ikiwa umefanya kosa lolote na uko karibu kuomba msamaha ni vizuri uanze na neno “Pole”. Neno hili inaweza kutumika kwa neno pi “Naomba msamaha” kuelezea lile kosa ulichofanya.

10. Kunradhi

Kunradhi ni neno la heshima inapotamka kupewa nafasi ya kuumndhi mwingine. Neno hili si kali sana bali inatumika kuonyesha kwa heshima ikiwa watu wamekoseana na kujaribu kuwa na mahusiano.

11. Niwie radhi

Neno lingine inaweza tumika kuomba msahama isipokuwa neno “pole” tu, neno sahihi kabisa ni neno “Niwie radhi”. Ukiwa umekosoa ama una jambo fulani kuonyesha kuwa unaweza omba msamaha kwa mtu yeyote, Niwie radhi ndio neno sahihi.

12. Naam

Iwapo mtu anayeitwa na anatak kuitika, Jibu sahihi ni “Naam”. “Naam” ndio jibu sahihi kwa kuwa ni neno inalotumika kwa heshima. Isiwe unajibu tu ovyo ovyo.

13. Shukrani.

Unaposaidiwa na mtu au unapo saidia mtu, neno “shukrani” hutumika sana sana. Iki fupishwa inaweza semwa “shukran”.

14. Simile.

“Simile” ni neno linalotumika na kutajwa mbele ya watu wengine ili upewe nafasi ya kujieleza kwa lengo unataka kutoa mbele ya watu.

Similar Posts