Aina za fasihi na maana yake

Fasihi ni sanaa ya lugha yaani ujumbe hupitishwa kwa njia ya kisanaa.

–        sanaa ni kazi ya mtunzi yeyote anayetumia lugha kupitisha ujumbe.

–        Fasihi ni kioo cha jamii ambapo maisha na tabia ya mwanadamu huangaziwa kisiasa, kiuchumi, kijamii.

silhouette of woman at blue sea inside black cave during daytime
Photo by Jens on Pexels.com

Aina za fasihi.

Fasihi simulizi – ni sanaa ya lugha inayowasilishwa kwa njia ya mdomo katika kizazi kimoja hadi kingine m.f;

–        hadithi

–        semi.

–        Nyimbe

–        Maigizo

–        Ngomezi.

Fasihi Andishi – ni sanaa ya lugha ambayo imeandikwa vitabuni. Kwa mfano; Riwaya.

Dhima ya fasihi.

1.   Huburudisha – fasihi hubutundisha kupitia nyimbo, hadithi na hata masharti.

2.   Huelimisha – mtu anaweza kujifunza mambo mengi.

3.   Hukuza uwezo wa kufikiria – mafumbo na vitendawili.

4.   Hukuza za maadili – methali.

5.   Hukuza usanii na ufasaha wa lugha – semi, methali na ulumbi.

6.   Huonga na kushauri – hadithi na masharti.

7.   Huelekeza – hadhira au wasomaji huelekezwa jinsi ya kuakabiliana na mambo.

8.   Hufahamisha na kujulisha kuhusu mazingira.

9.   Huendeleza utamaduni – mila hudumishwa kupitwa kwa kazi za fasihi kama vile nyimbo na hadithi.

Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi.

Fasihi simulizi.

1.   hii ni mali ya jamii nzima.

2.   Ni rahisi kusahaulika na kuvurugika kwasababu ni ya kupokezana na huhifadhiwa akilini.

3.   Huweza kubadilishwa wakati wowotw ule ambao msimalizi anawasilisha.

4.   Haina hadhifa mahsusi.

5.   Hadhira au wasikilizaji huadhiriwa uwasilishaji.

6.   Hadira au wasikilizaji huhusishwa katika uwasilishaji wa fasihi hii.

7.    Uzuri wa kazi hizi kutegemea anayewasilisha.

Fasihi andishi.

1.   Hii ni mali ya mtu binafsi.

2.   Mahifadhiwa kimaandishi hivyo basi si rahis kusahaulika wala kuvurugika.

3.   Si rahisi kubadilishwa.

4.   Hadhira yake ni mahksi.

5.   Hadira au wasomaji hawana mchango wa moja kwa moja katika kazi hii.

6.   Kazi hizi zimeandikwa hivyo basi hadhira au wasikilizaji hawahusishwi kamwe katika kazi hii.

7.   Uzuri wa kazi hii hutegemea wa mwandishi.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts