Ilikuwa sato, ambapo niliamka asubuhi kupata Mkoro wangu alishakuwa ameenda kazi. Kwa meza niliachiwa doe ninunue oredho kwa duka. Nilienda polepole kwa duka nikabuy, nikarudi kejani ktulia tu nikiwatch movie fulani ya dj afro.
Category: Insha

Familia yangu inahusu na watu watano. Hawa ni baba,mama,ndugu na Mimi. Jina la baba yangu ni Joseph otieno. Yeye ni mrefu na mwembamba kama sindano. Yeye hufanya kazi Kwa kampuni ya middemb. Yeye hufanya kazi sana ili Mimi na ndugu yangu na dada yangu tupate kula na tupate mavazi.

Nilirauka rau rau baada ya jogoo. Nilienda bafuni kama maji ilinitiririka tiri tiri iliyokuwa maji baridi shadidi. Nilipomaliza, nilienda kuvaa nguo nilizopendeza sana

ulikuwa mwendo wa saa tatu jioni, mama alipoingia nyumbani huku uso wake ukionyesha furaha. Nikauliza nini inafanya yeye awe na furaha hivi. Mama aliniangalia na kusema keshi ni harusi ya mjomba wake. Mama alileta nguo zina na madoa kwake na kuniletea nguo nzuri ilyokuwa suti.

Lakini wazazi wangu hawakuwa na karo ya kutosha kwa kuenda shule niliyotarajia. Nilishikwa na huzuni sana kwamba machozi yalinitoka nikifikiria vile nitapanga kuwa na maisha mazuri kwa maisha yangu ya kesho. sikutaka kuwa maskini ama maisha yawe mgumu kwangu.

Jini Hilo liliponieleza hayo, lilipotea Nami nikajikuta nyumbani. Sikuamini Yale niliyoyagundua lakini nilinyamaza kimya na kutulia tuli laiti ningaligundua tabia ya Siri ya babu kabla Aage Dunia. Ningalimwelezea kuwa kumla nguru si kazi, kazi kumwosha.

Ilikuwa ijumaa moja nilipodamka bukurala, tayari kwenda kazini. Baada ya kustaftahi, nilijikwatua kwatu kwatu na kuenda kazini. Kazi yangu ilikuwa ya kuwanasa mapwagu na mapwaguzi wa Jiji la Nairobi wezi wote waliniogopa kwani hakuna hata mmoja aliyetoroka kutoka mikononi mwangu.

Kazi yangu ilikuwa ya kuwanasa mapwagu na mapwaguzi jijini Nairobi. Nilikuwa mtu mashuhuri sana. Mabwanyenye Kwa watumwa walinipongeza Kwa kazi yangu njema ya kuwanasa wezi na wanyangani. Waligua hakwaa mwizi alitoka mikononi wangu. Nilifanya kazi yangu Kwa udi na uvumba Hadi wezi waliaadimika kama wali wa daku.

Teknolojia imeleta vitu vipya kama simu,Tarakilishi na vinginevyo. Teknolojia imesaidia kila mtu na kila mahali. Vitabu sana, maisha hayakuwa rahisi. Watu walikuwa wakitembea Kwa miguu wakienda kusafiri mbali sana. Pia walikuwa wanatembea Kwa miguu tupu kila mahali. Watoto sana sana kusoma , walisoma Kwa shule zilizoporomika au Haina mjengo wowote

Nilivaa nguo zangu nikinywa chai kwa mkate iliyokuwa tamu kama asali. Nilipomaliza, nilianza safari kwenda shuleni. Siku hiyo ilikuwa siku ya mwisho ya muhula wa kwanza. Nilipofika shuleni wazazi walikaribishwa na kuketi kwa viti vilivyokuwa nyeusi tititi.