Hadithi fupi – ya mapenzi mahaba chiku.

Naam hii ni hadithi fupi kuhusu msichana mrembo amabaye alillelewa mjini wa Kasriba pamoja na wazazi wake wawili, ambao alimsomesha chiku kutoka chekechea hadi chuo kikuu na kufaulu kupata kazi mjini Nairobi.

Chiku alikuwa na mpenziwe anayeitwa joseph ambaye walipendana sana tangu shuleni ya upili. lakini maish ya joseph yalikuwa yakunga’ng’ana. Joseph amekuwa akifanya juu chini kupata kazi ambayo itampa maisha bora na pia kuweza kuishi na chiku mpenziwe wake wa kufa kupona na hata hivyo kumwoa na kufunga pingu ya maisha.

Lakini vile maisha ni magumu mno, amejaribu kufanya kazi analolipata ya kujiskuma maisha. Joseph kwa kweli akona ndoto, ndoto ya maisha bora na chiku, lakini kwa sahii kwa hali yake anomba mola amsaidie.

Chiku anafanya kazi katika benki ambaye yeye ni sekretari. Amefanya kazi huko kwa muda wa miaka miwili. Kwa kweli anajua joseph anafanya juu chini kupata kazi bora, chuki ana imani kuwa joseph atapata baraka yake na ombi lake mola atatimiza.

close up photo of two person s holding hands
Photo by Git Stephen Gitau on Pexels.com

Chiku anaishi ana pekee yake jijini nairobi, na pia joseph anaishi pekee kwa jumba lake la mabati sio mbaya vile, lakini chiku jumba lake ni la gorofa. Si eti wawezi ishi pamoja lakini kwa Joseph itakuwa aibu kwake kuishi kwa nyumba ya mpenzi wake. Joseph aliamini kuwa, heri mkewe aishi kwako.

lakini kwa hii hadithi, ni maisha ya chiku ndo tutasimulia sana, kwa vile, chiku si chiku tu bali pia ni msichana mwenye bidii. Hii ni hadithi fupi ya chiku na maisha yake.

” Good morning good morning….. nairobi its 6 in the morning…”

Chiku anarauka asubuhi na mapema na kujitayarisha kuenda kazini akisikiliza redio. Aliposikiza ni saa ngapi alihisi kwamba anaweza chelewa. Kwa kasi aliingia bafuni kuoga na alipomaliza alijipikia chamsha kinywa na kuvaa mavazi yake na kuangalia kila kitu kwa nyumba kama iko sawa.

Kwa simu yake akaangalia ni saa ngapi….. 7:00 am ” wah… si na chelewa leo.”

alichukuwa vifungu zake za nyumba na kuifunga kwa kufuli. Kisha akaanza safari yake kazini. Njiani akapata basi la abiria. ” beba beba bea tao tao…. madam unaenda ama.” Chiku akaiingia kwenye basi hilo na kuendelea safari hiyo.

Kwa mshangao, kulikuwa na msongamano wa magari. Hii ilimpa chiku wasiwasi. kwa dakika thelathini hivi, alifika kazini kama amechelewa. Kwa mkoba wake akatoa simu yake kuona ni saa ngapi. kwa simu iliandika 8:30 am. ” wah am late.”

Chiku aliingia kwa ofisi lake mahali anafanya kazi na kukaa kwenye kiti na mezani wake. Mbele ya ke ilikuwa komyuta ambao aliwasha na kuongoja aitumiwe. ghafla bin vuu aliskia sauti ya mtu akibisha mlango.

” Hodi…”

” Karibu.” chiku akajibu.

mwenye alibisha mlango ilikuwa mkubwa wake wa kampuni anayeitwa Erick. Mwajiriwa, alingia ofisi wa chiku na akauliza.

” Ni saa ngapi sasa hivi unaingia ofisini?.”

” Pole sana mkubwa, i will not repeat it again.” Chiku akasema.

” Kwani leo shida ilikuwa nini?.”

” ni……. ni msongamano wa magari.”

” Kwsho uje mapema, na nisikupate ukichelewa tena, tunaelewana.”

” Ndio boss.”

” Good endelea na kazi.”

Erick alitoka ofisi wa chiku na kuenda zake. Chiku aka kaa kutlia kidogo ndo aanze kazi yake, kuona hivi tarakilishi yake inaakaa kwa muda mrefu kufanya kazi.

***************************************

Joseph aliamka asubuhi kama amechangamka. Kwa mlango akasikia sauti ya mtu ambaye anajaribu kufunga mlango na kufuli. Joseph alikimbilia kwa mlango na kusema.

” weh…. huyo ni nani?.

” Ni caretaker, lipa kodi ama nikufungulie ndani.”

joseph katoka inje kwa kasi na kujaribu kuongea na caretaker.

” caretaker usikuwe hivo si nilisema nitakulipa…”

” Tangu lini utanilipa joseph, imekuwa miezi mitatu na bado hujanipa hata pesa kidogo, leo ni leo itabidii uhame au nitafunga hii nyumba.” caretaker akasema.

” Caretaker basi leo jioni nitakulipa, usiwe hivo.”

” Leo, uko sure, leo?.”

” Ndio mimi joseph, nitakulpia full cash.”

” leo nakuruhusu leo tu…… joseph sawa.”

Caretaker mwenyewe akatembea kuenda zake akiwa na vifungu mikononi mwake.

Joseph akaingia ndani ya nyumba yake na kujitayarisha kwenda kufanya kazi yake. Akachukua kifuli chake na kufunga nyumba yake na kuanza kwenda kufanya kazi kwa duka. Joseph alipewa kazi ya kuuza bidhaa ya duka ya mkubwa wake. kutoka asubuhu saa moja asubuhi mpaka saa kumi na tatu usiku.

Wateja wakiwa wengi, ilikuwa siku nzuri kwake kwani pesa inakuja kwa wingi na pia ana weza kulipwa vizuri mwisho wa mwaka. Ikiwa wateja si wengi, ilikuwa hasara kwake.

Na pia alikuwa anatafuta kazi kila wikendi lakini hakuna aliyempigia kumpa kazi. na kazi hili la duka ndio ilikuwa tegemeo lake.

” Ehh joseph.” mkubwa wake akamwita.

” ndio..” joseph akamjibu.

” EEh shika hii pesa kwa leo, najua biashara haijakuwa vizuri lakini nitakulipa yote badaye.”

” haina shida.” joseph akasema.

” leo pumzika kidogo…. nitachukua kuotoka hapa na kesho uje mapema sawa.”

” sawa… asanti sana.”

************************

Ilikuwa saa kumi na moja na joseph alikuwa karibu kuenda nyumbani na akakumbuka kumpigia chiku wapatane kidogo. Alipofanya hivo, walikuwa wapatane saa kumi na moja unusu katika hoteli fulani.

Joseph alifika wa kwanza na kuongojea chiku afike. kwa muda alikuwa ametulia tuli akinywa chai na kuoma gazeti. Haikuwa kawaida yake kusoma gazeti lakini alikuwa ameboeka akaona anunue gazeti la kusoma.

Alipomalizia kusoma gazeti, aliona chiku akija pole pole na kumtafuta. Joseph akanyoosha mkono na chiku akamwona. Chiku alipomwona joseph, alikuwa kwa furha buraha akiketi kwa kiti.

” Ulikuwa umepotea?.” joseph akasema.

” hapana, kukutafuta tu.” Chiku akamjibu.

” Naona leo umevalia vizuri, kazi imekupeleka aje.”

” Huskii leo nilichelewa…. mara yangu ya kwanza.”

” Usijali, there first time for everything.”

” Si kawaida langu.” chiku akasema.

” Ulipatikana?.” Joseph akauliza.

” Ndio na mkubwa wangu, nilikuwa nimeshtuka.”

Mhudumu aka tokelezea, na kuwauliza.

” Hello, niwalete nini?.”

” Ningependa chai tu na mandazi miwili hivi.” Chiku akasema.

” Kile yeye ana kula mimi nitachukua.” Joseph.

” sawa basi… mtanipa dakika tu tano itakuwa tayari.” Mhudumu akasema.

” Hakuna shida”, chiku akasema.

mhudumu akaelekea jikoni, hapa chiku na joseph akaendelea kuongea.

” Joseph, mambo ya nyumba je?.”

joseph aka kaa vizuri na kimya na kujibu.

” Iko tu sawa. mambo yako shwari.”

” Joseph ?.”

” Uswiwe na wasiwasi, mambo yatakuwa shwari.”

” Aje shwari na utalala inje?.”

” Sitalala inje.”

” wapi surely. Isipokuwa kwangu ulikataa kuishi.”

” si….unajua sababu?.”

” Ndio nilielewa sababu lakini je utalala wapi?”.

Mhudumu akafika na chai miwili, mandazi nne na kueka mezani yao.

” Asante.” chiku akasema.

” Karibu.” Mhudumu akajibu.

chiku akangalia joseph kwa makini akiwa anayanywa chai yake.

” Joseph jibu?.” chiku.

” Usijali all will be well.” joseph akila andazi.

” Kazi ilikuwa aje?.”

” Si mbaya, ila nilishtuka leo mkubwa aliniachilia mapema leo.”

” Ndo nilishangaa leo mbona umenipigia leo.”

” Yes at least to see you.”

” Kuwa mda mrefu ku kuona.”

” I missed you.”

” Missed you to.” Huku chiku akitabasamu.

Mhudumu alirudi akiwa na risiti, na kuchukua vikombe na sahani iliyokuwa kwa mezani yao. Joseph akalipia bill. Chiku na joseph wakaanza kutembea kuelekea kwa steji ya mabasi kuelekea nyumbani yao.

walitembea pamoja wakiwa wameshikana mikono wakiongea, kutembea kwa mwendo usiokuwa mbio sana, na sio polepole sana. Wakiwa karibu kwa steji ya basi chiku alisimama na joseph akasimama pia.

” Joseph?.” chiku akasema.

” Yes?.” Joseph akamjibu.

” Tunaweza cheka na wewe na leo usiku iwe una lala aje.”

” Usijali…… niko sawa.”

” Hapana, hauko sawa.” chiku akingia kwa mkoba wake na kutoa bahasha.

” Hii nini ?.” Joseph akauliza.

” Hii ni 5000 cash, shika sitaki leo ulale inje.” akimpa kwa mikono zake.

” aaah chiku hapana am okay.”

” Joseph chukua ujisadie….. sitaki nikuone hapa inje unalala hauko sawa.”

” ………….hapana we kaaa nayo uitumie vile unataka.”

” Joseph ukitaka kuniona tena……….chukua hii bahasha.”

Joseph akatulia kwa muda kidogo, na kiuchukuwa bahasha hilo.

” Nitakulipa, i promise.”

” Si deni Joseph……..”

Chuki akamkubatia joseph, na kumwambia.

” Take care…… sawa.”

” safe journey my dear.”

Chiku alipanda basi na kupunga mkono joseph basi iking’oa nanga.

********************************************

Usiku ilifika na care taker alikuwa kwa mlango ya nyumba ya joseph. Caretaker alingojea joseph kwa hamu na ghamu. Joseph alitokelezea na kuona caretaker mbele yake.

Caretaker ” Ahadi ni deni…… nilisema leo ni leo.”

Joseph akaingiza mkono wake kwa mfukoni mwake na kutoa bahasha na kumpa caretaker.

” Five thousand……. ndio hiyo.” joseph.

care taker akatabasamu. na kusema.

” uwe ukifanya hivo, na hatutasumbuana.”

Joseph alingia kwa nyumba yake. Aliketi kwa kiti chake akiangalia paa. Hakuamini kile chiku alichomfanyia. Ilikuwa fikra iliyokuwa kichwani yake. Na usiku hiyo hakuwa na usingizi mno.

to be continued……..

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts