Hadithi fupi ya siku ya mganga.
Naam, kwa kuwa katika michezo ya kandanda kulikuwa na timu ya “wakali ndio sisi.” Ambapo Kila saa walikuwa wakishindwa katika michezo yao Kila wakati.

Ndio walikuwa na bidii za mchwa na walifanya juu chini kufanya zoezi inayofaa. Isikose kochi wao alikuwa Simba. Mkali mno anapongea wachezaji wake wanaogofya. Lakini kochi huy hakuelewa mbona Kila wakati timu yao inashindwa Kila mechi unaofanyika.
Siku Moja kochi huyu ambaye tutamwita George alitafuta sululisho lingine ya kusaidia kutengeneza tatizo hiyo. George alitembea kando ya Barbara akapata posti limeandikwa ” mganga mjanja kutoka mbali…” Pamoja na nambari ya Simu.
Ghafla bin buy George aliandika nambari huo kwa karatasi na kuipiga nambari huo.
George: hello.
Mganga: sema shida lako ni kusaidie vipi.
George: hii ni nambari ya mganga?
Mganga: ndio, sema tatizo lako unanipotezea wakati.
George: tatizo langu ni kuwa, nikona timu ambaye nimefanya juu chini ili ifaulu lakini kila siku nikijaribu na feli.
Mganga: aah hiyo tu, usijali kuja kesho katika msitu wa mbali…. ukifika hapo nitakushugulia.
George: sawa, utanipata, kesho saa ngapi?.
Mganga: saa mbili asubuhi, usichelewe.
George: sawa basi.
George aliendelea kutembea hadi nyumbani, na kufika mapema ili ajitayarishe kwenda mgagaa huyu ambaye atatiza matatizo lake. Jambo hili kwa kweli ilimkera george na aliamini sana kuwa ndio tatizo itapatikana kusaidia vijana wake wafaulu kwa mechi zijayo.
siku aliyoongojea, ulifika. George aliamka asubuhi na mapema kabla ya jogoo kuwika. Alivalia mavazi lake na kuenda kuelekea kuona mgagaa huyu. Alitembea kwa kasi kuenda msitu mbali. Alipofika, aliingia kwa msitu huu, na kupiga simu kuuliza pale huyu mgagaa yupo.
George: hello… nimefika.
Mganga: umefika, wacha nikuje pale uko, na kuona.
George hakuwa na uoga, alikuwa akimgoja mganga huyu kwa hamu na ghamu, na kile aliotarajia, ilikuwa mshtuko mno. Aliona mganga huyu akiwa amevalia shuka nyekundu, akiwa na fimbo mkononi mwake wa kushoto. Akiwa akokaribu kukaribia, George alihisi kuwa anatambua mtu huyo. Alipofika karibu Mganga huyu alishtuka mno, na kwa mshangao akasema
Mganga: george?.
George: kevoh?.
Mganga: george unfanya nini hapa?.
George: si nimekuja kuona mganga.
Mganga: huyo mganga ni mimi basi.
George: lakini wewe si ndugu yangu?.
Mganga: ndio, lakini……
George: lakini nini.
Mganga: lazima uwe mjanja ndio upate pesa.
George: lakini si namna hivi.
kevoh alikaribia george na kumwambia
Mganga: huku, in the city, lazima uwe mjanja, maisha hapa inje si rahisi. hakuna kazi.
George hakuamini kuwa ndugu yake anaweza kuwa mganga ili apate pesa. George na ndugu yake mganga walitembea pamoja, wakipiga gumzo kuenda nyumbani. Kwa kweli kile george alitarajia, si ile kuwa ndugu yake ni Mganga.