Hadithi ya mahaba.(story of love.)

Sijui niseme aje, kwamba hii ni ndoto ama tuu ni fikra zangu akilini. Niliota kuwa nilikuwa ndani jijini wa nairobi, watu wakitembea kuenda kivyao hapa nikiwa nimesimama. Sijui sababu langu ya kusimama katika jiji ambapo watuwengi mno na kuwa ukisimama unagongwa, na kupewa macho makali kana kwamba mimi ndo makosa nimefanya.

red flower on white sand
Photo by How Far From Home on Pexels.com

lakini kusimama hivi ilikuwa na sababu fulani. Sababu hili ni kuwa ni kama natafuta mtu kati ya hao watu wengi mjini. Magri yalipita, mahoni ilisikika, magorofa kubwa ni hayo tu niliyaona. Lakini kuna vile macho yangu yakapatana, na mtu moja ambapo mpaka roho yangu ikaanza kudonda.

Vile nilihisi, nilipomwona pia yeye kwa mshangao aliniona na akawa na furaha kuiniona kwa umbali kati ya watu wengi. Nilipofumba na kufumbua macho alipotea. NIlistuka mno nikawa nikaanza kutembea kumtafuta, kidogo kidogo, nikaanza kukimbia kumtafuta. Kidogo kidogo nikagundua kuwa ni ndoto niliota.

Mama Alfred: amka, amka jameni tutachelewa kuenda mashambani.

Alfred: aahhh mam jameni, leo mapema asubuhi hii?.

Mama Alfred: Mimi nilikuambia usilale mapema?. shauri yako jitayarishe twa chelewa.

Mama Alfred na Alfred walielekea shambani kubwa ya majani chai, kufanya kazi ili wapate mapato yao ya kila siku. Mama Alfred amekuwa akifanya kazi huko kwa miaka kumi mno.

kufika shambani huo, walipata wakubwa wakitembea kuangalia shambani yao. Kuona hivi kilileta mshangao kwa mama alfred ambaye hakuwa na habari au kujua kuwa wakubwa wa shambani hili watarejea.

Mkubwa moja: mama alfred, how are you?.

Mama alfred: am fine boss.

Mkubwa huyo akangalia alfred, kwa furaha yake akasema.

” Alfred how are you?.

” fine sir.”

“umekuwa mkubwa, najua ukiwa mdogo nilikubeba, lakini sidhani unanikumbuka.”

” Ah kweli, labda na kumbuka.

” Amemaliza masomo yake ya shule ya upili sasa hivi anahitaji kuenda chuo kikuu.” Mama alfred akasema.

” ah kweli hiyo ni nzuri, i want to intruduce you to my daughter Natalie.

Natalie katokezea kusalimu mama alfred pamoja na alfred mwenyewe. Alfred alipomwona Natalie kuna vile anahisia hajawahi kuwa nayo. Kumwona msichana huyu ambye alikuwa mrembona mweupe kama theluji.

” Ahh this is natalie, amekuwa mkubwa.” mama alfred akasema.

” kweli kweli, am wacha leo nitembe kuchunguza mambo ya shamba alafu tutaongea baadaye.”

” sawa boss, wacha sisi tufanye kazi.”

Natalie na babake wakaenda kutembea kuchunguza shamba lao, hapa mama alfred na alfred mwenyewe wakaendelea kufanya kazi yao ya kuchuna majani. Katika shamba hili ilikuwa ya majani chai ya ma acre kubwa sana na kazi hii si rahisi mno. Kuwa ilikuwa muhimu sana kufanya kazi asubuhi kabla jua ya saa saba kuchomoza ije ichomoze mgongo yao.

Alfred na mama yake walifanya kazi yao kwa bidii karibu saa zote hadi kupumzika kwao ikawa saa tisa hadi saa nane na kuendelea kazi yao hadi saa kumi na moja. Saa kumi na moja ilipoelekea, Mama Alfred na Alfred walianza kujitayarisha kuenda nyumbani.

” Alfred, si uende ununue gunia hapa tu alafu ukirudi tuanze safari yetu kuenda nyumbani.” mama alfred akasema.

” sawa mama, wataka ninunue ngapi?.”

” Nunua tu ya hayo pesa, fanya haraka hatuna muda.”

Alfred akchukua pesa na kuanza kukimbia kwa kasi mno ili kununua gunia hili. Kwa njiani ambapo mbele yake kwa umbali kulikuwa na duka, uliokuwa pekee yake katika shamba hilo. Alipoelekea kufika dukani, kwa bahati mbaya Alfred alitegwa na mawe njiani na kuanguka chini sakafuni pu.

kujaribu kuamka akaona mkono ikinyoosha mbele yake. Alfred alinyoosha mkono wake na kusaidiwa kuamka. Kwa mshangao wake akaona kuwa ni natalie ndio amemsidia kumwa amsha ili asimame.

” Pole jamani uko sawa?.”

” niko sawa…. asante.”

” uko sure?.”

” Am sure.”

” But you are bleeding on your knees.”

” si jambo kubwa sana….”

” na mbona unakimbia kwa kasi hivo?.

” Nilikuwa nimetumwa, ninunue gunia, na tunachelewa.”

“hukuniambia jina lako.”

“Jina langu?, jina langu ni Alfred.” akinyoosha mkono kumsalimia.

” Hadi ushajua yangu, Natalie.”

” Nice to meet you natalie… lakini ningefaa kukimbia muda unakimbia.”

” Basi jichunge, usikajiumize.

alfred akakimbia kununua gunia aliotumiwa akanunue na mama. Alipopata, aliona kwa umbali natalie na babake wakingia kwa gari ya kifahari ya prado V8. Alfred alikimbia kuelekea kwa mama yake ndio wa anze safari kuenda nyumabani.

” Ah Alfred ni nini iliganyika?.”

” nilianguka tu mama si jambo kubwa.”

” Nawe pia, unakimbia aje hadi unanguka chini kwani huoni pahali unaenda?.

” Ah mama, man is to error.”

” EBu twende nyumbani twachelewa, next time chunga mahali unapoenda.”

Mama Alfred na alfred wakaanza safari kuenda nyumbani. Lakini kwa masaa hizi hawa kuwa na haraka, pole pole tu ndio mwendo wakinunua ugali na mboga, kutayarisha chakula yao ya usiku. Kwa kweli kwa akili ya Alfred ilimshangaza ni kuhusu Natalie, lakini hakufikiria sana kwani ana kazi mengi kwa nyumba. Lakini hii ndo siku ya kwanza alipomwona na kumtambua.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts