Insha kuhusu jirani yangu

David ni jirani yangu mpendwa anayeishi katika karibu nyumbani kwetu. Nilipohamia hapa miaka mitatu ijayo, David mwenyewe alinikaribisha hapa kuonyesha vile mtaa wa huku karibuni inakaa. Anapendeza sana kuwa na jirani kama yeye kwa sababu ni mtu mzuri na mwenye moyo wa ukarimu.

new home
Photo by Soly Moses on Pexels.com

David ni mtu mwenye mwangalifu sana na pia tunaweza sema ni mtu mwenye tabasamu la kuvutia sana. Kwa heshima na adabu kwa vile ni mtu wa kutabasamu watu usoni, anapenda kusalimia watu kujua na kujali hali yao na mahitaji yao ikiwa akona suluhisho anaweza saidia mtu.

Pia kwa hayo yote, David ni mtu mwenye ukarimu usio na kifani. Mara kwa mara ni mtu amenisaidi na mambo mengi ya mbali mbali. Kwa mfano, mara moja nilikuwa na tatizo na gari langu na nilihitaji msaada wa haraka. Bila kusita, David alinipa lifti na kuniendesha hadi kwenye gereji ili nipate msaada. Hilo lilinivutia sana na nilifurahi kujua kwamba naweza kumtegemea wakati wa shida.

Jambo lingine kuhusu David ni kuwa ana talanta nyingi. David ana uwezo wa kucheza muziki kwa vile anapenda kutumia gitaa lake nyumbani mahali ambapo analifanyia mazoezi yake. Na kwa hiyo Talanta yake imempa faida nyingi ya kuwafunza wanafunzi wake jinsi ya kucheza gitaa na wengi wamepata ujuzi mzuri chini ya uongozi yake.

Na kitu kingine kuhusu David ni upendo wake kwa wanyama. David ana kipenzi chake mbwa anayeitwa Ray Ray. Mara kwa mara akona muda wake kati ya yeye na Ray Ray ambapo anamtemebeza katika bustani yetu ili aweze kushirikiana na watoto. Haya yote inaleta furaha kwa watoto walio karibu.

Ikikuja kwa mikutano, David huwa mtu wa nidhamu. Mara nyingi amekuwa akihudhuria mikutano ya jumuiya yetu na anatoa mchango yake katika kuboresha maisha ya kijamii. Amesisitiza mara nyingi kuwa kuishi kwa amani na upendo inaleta jamii pamoja.

Kwa kumalizia, David ni jirani ambaye nina bahati kumiliki. Ana tabia nzuri, ukarimu, talanta, upendo kwa wanyama, na nidhamu. Nafurahi sana kumpata David kuwa jirani yangu, na ninaamini kwamba uhusiano wetu utadumu kwa muda mrefu. Ni mfano bora wa jirani anayeweza kuwa na ninajivunia kuwa na jirani kama yeye.

Similar Posts