Insha kuhusu mwizi au wezi

Ilikuwa ijumaa moja nilipodamka bukurala, tayari kwenda kazini. Baada ya kustaftahi, nilijikwatua kwatu kwatu na kuenda kazini. Kazi yangu ilikuwa ya kuwanasa mapwagu na mapwaguzi wa Jiji la Nairobi wezi wote waliniogopa kwani hakuna hata mmoja aliyetoroka kutoka mikononi mwangu.
Nilipata Raha na buraha nilipomshika mwizi mmoja wa genge kwani nilijua vyema ya kuwa pwagu humshika pwaguzi. Mmoja baada ya mwingine wezi walinaswa Hadi wizi ukaadimika kama wali wa daku jijini Nairobi. Wanachi wote, wakubwa Kwa wadogo . Mabwanyenye Kwa watumwa walinishukuu Kwa kazi yangu njema. Mimi Nani nilitabasamu kwani nilipata Raha kama swara aliyevumburushwa nilipoona matunda ya kazi yangu. Chembilache wahenga. Kile unachopanda ndicho utakachovuna.
Ijumaa hiyo ya baridi. Niliwahi kazini kuchelewa kidogo kwani manyunyu ya mvua yalinisababisha niende Kwa mwendo wa lumbwi.
Sikuwa nimejiketisha niliposikia simu ikilia. Niliichukua bila kuchelewa na kuuliza ni nani aliyekuwa akinipigia. ” Jina langu ni Juma!. Sauti ya kunguruma ilinena.” Nimemwona mmoja wa wezi wa genge mashuhuri la Almasi hapa Kariobangi. Tafadhali Fanya Halahala au sivyo, utapata mwana si wako.
Niliweka simu chini bila kusita na kuazima gari la sahibu wangu wa udi na uvumba, Ali. Aliponipatia gari lake, niliitoa. Mbio mithili ya risasi Hadi Kariobangi. Nilipofika huko. Nilitoka garini na kupepesa macho yangu huku na kule.
Genge la Almasi lilikuwa genge mashuhuri la wezi na wanyangani. Lilikuwa na washirika kumi na wanne wenye miraba minne. Wote walijaa misuli kila mahali na walikuwa na sauti za kungurumisha nchi.
Nilikuwa nimejaribu kuwashika wezi wa genge Hilo lakini wapi ! Kila nilipojaribu niliambulia patupu. Hata hivyo, sikukata tamaa wala kugota.
Nilitoa bastola yangu mtu Koni na kungia kwenye klabu mashuhuri mtaani humo.Nilipoingia, kila mtu aliniangalia Hadi nikafedheka. Nilirudisha bunduki yangu mtukoni na kuenedelea kutafuta.
Ingawa nilikuwa nimekula chumvi nyingi sikuwa mtu wa kuchoka haraka. Watu wengi waliniambia ning’atuke lakini nilizidi kujitoa mhanga ili kuwanasa wezi.
Katika harakati zangu za kutafuta maskani ya wale mapwagu, nilipigwa butwaa chakari kumwona mmoja wao akishikilia bunduki, tayari kuniua!.
Lo! Nishtuka sana na kuruka nyumba ya gari moja lilikuwa kando ya baraste. Ndipo mwizi huyo alianza kufyatua risasi kama mwehu aliyetoroka kula kalendaa. Mimi Nami siku mwacha. Nilimfyatulua risasi nikitarajia kumpeleka ahera bila nauli lakini sikufua dafu.
Muda si muda, genge lote la wezi lilijitokeza na kunizingira Kwa kila upande. Kabla ya kupumua mara tatu , niliskia uchungu chuma kisogoru mwangu na nikazimia zii, nilipoamka nilijikuta nimelala Chali, huku nimezungukwa na genge la wezi.
This a good work
Thanks