insha kuhusu ndoto ya ajabu.

Nilikuwa ndani ya nyumba nikiona kwa dirisha kwa kuwa mvua ilikuwa inatiririka kutoka mbingu lakini haikuendelea sana vile. Asubuhi hili lilikuwa inanichenga. Nikitoka inataka kunyesha, nikirudi hainyeshi. Baada ya masaa kidogo tu mvua uliacha kunyesha, nikaanza kujitayarisha kwenda kanisani.

grayscale photo of wrecked car parked outside
Photo by Aleksandr Neplokhov on Pexels.com

Nilipotoka inje, jua lilikuwa ndi kwanza linajitahidi kutokeza myuma ya mawingu yaliyotanda anagani. Lilifanya hivi kwa hadhari kama mtoto asiyejua afanye jambo alilokatazwa au la. Mvua iliyokuwa nyepesi iliacha vidimbwi vya maji machafu hapa na pale kando ya barabara za jiji la Nairobi.

Matope haya yalinizidi na nika tafuta gari la texi, iwe mbinu yangu ya kwenda kanisani nisichelewe. Nililipata gari na kwenda kuelekea kanisani. Hapa kama kawaida kila jumapili na kwenda kukipokea chakula cha kiroho. Lakini hapa nilitaka Mwenyezi mungu anifungulie njia ya kunisaidia nipate riziki ili ni pate pesa ya kusaidia dada langu amalize shule.

Dada langu Rita alikuwa kidato cha nne na mtihani ulikuwa karibu. Akili yangu Ilizongwa na fikra ya kupata karo yake ili amalize. Nilifanya juu chini kutafuta kazini mjini huu Nairobi lakini niliambulia patupu. Si kufa moyo. Nilishuka mbele ya kanisani nikapatana na rafiki yangu wa kufa kupona.

Halima ambaye tumejuana sana kutoka tuwe wadogo alijitokeza na tukaaingia na yeye ndani kanisani. Muda iliyochukuwa kwa kanisani haikuwa sana mno. Saa ilipomaliza ya kanisa nilienda kwa kasisi kueleza usaidizi kidogo tu na kumwelezea shida langu. Alinisikiliza na kunisaidia pesa za karo ya shule ya dadangu Rita.

Nilimshukuru sana. Alinishauri niwe mwema na nikiwa na shida lolote niwe namwambia. Nilipotoka kwa ofisi la kasisi, nilimwona halima akiningoja. ” kwani ulikuwa unanigonja?.” niliuliza. ” ndio.’ hivo ndio alinijibu. Tulitembea na kuongea pamoja kuelekea nyumbani lakini kwa mwendo wa asteaste.

” Unaweza niingoja hapa, nataka kununua kitu dukani.” halima alisema.”ndio.” nikajibu. Halima alijaribu kuvuka barabara ili aende akanunue kitu alichotaka, ghafla bin vuu sikuamini kile nilichoona. Niliona barabarani Halima akipigwa dafrao na gari jikubwa ya aina ya Range rover.

Nilimkimbilia barabarani hapa Waraia wakizunguka gari hilo wakimpuuza dereva huo. Damu yalikuwa kichwani ya Halima nikalilia usaidizi wa kumbeba. Waraia wengine walinisaidia kumbeba Halima hadi kiti la nyuma la Range rover hilo.

Dereva huo alikuwa kwa mshangao, akijishika kichwani. ” Nini wewe, endesha tumpeleke hospitali.” Nilisema. ” Unaskia kila nimesema, wewe ziwi au nini?.” Dereva huyu alingia kwa gari lake na kuasha gari. Alitia gia na kuling’oa gari lake haraka na kuwacha risasi za matope kuwasiliba waraia nyuma yake nyusoni na kuwaacha kuwaacha wakilani na wengine walikuwa wakitema chini matope yaliyopenya kirisasi vinywani yao.

Halima alikuwa kwa mkononi wangu wangu hapa machozi yalinitoka ikitiririka tiritiriri. Moyo wangu ulinidunda dududu hapa nikimwambia halima aamke kwa sikio lake, asiniache niwe hivi. Tulifika kwa hospitali ya Mariakani tukaona madaktari wakitoka inje kuja kunisaidia kumbeba.

Alipelekwa ndani ya hospitali na kunionyesha mahali nitaketi. Shati langu ilijaa na damu ya Halima. Dereva huu aliniangalia na kusema pole kwa kugonga kwake. Tuliketi na kuongea na yeye, na alitoa ahadi kwamba atalipia bill yote ya hospitali kwa muda wa masaa mawili daktari moja alijitokeza akiwa amevaa miwani. Nilisimama imara, aksimama na kujaribu kuniambia hali ya halima. Kabla ya kufubgua domo lake, Niliamshwa na Halima mwenyewe. “Wewe amka kwani utalala hadi saa ngapi.” Halima alisema. Nilishtuka kumwona ” Nilidhani uko hospitali.”nilisema. ” Eti hospitali, wewe ulikuwa unaota wewe.” alisema. Na hivyo niligundua kwamba niliota ndoto ya ajabu.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts

One Comment

Comments are closed.