Insha ya ajali haina kinga.

Kuandaliwa kwa siku yenyewe kulikuwa kumeshakamilika na sikuamini itafanyika. Hivi ndio siku ilianza kwangu. Nilirauka raurau kabla ya bwana shamzi kupasua matlai yake. Nilienda hamamuni kucheza mchezo wa bata.

Toa mvuke kama chai moto, nilienda kuvalia nguo iliyonipendeza nyeupe pe pe pe na kunimeta metu metu. Kisha Nilienda sebuleni kuchukua kiamsha kinywa iliyokuwa tamu kama asali.

Nilipoangalia saa nilikuwa nachelewa na nilitoka shoti kutoka nyumbani na kuelekea kanisani. Nilingojea kwa hamu na ghamu nikingojea basi au matwana yoyote itakayo jitokeza.

nilipatana na rafiki yangu wa kufa kuzikana na tulipendana kama chanda na pete. Tuliongea kwa muda mfupi na kwa kweli kama singepatana na yeye ningekuwa kwa uchovu sana.

Rafiki yangu alinifurahisha kwani nilijawa na furaha mpwitompwito. Tulipoendelea kuongea, basi moja ulifika mbele yetu hapa viti vilikuwa vya kupendekeza, nyimbo zilizo za kidunia, ilikuwa na televisheni ndogo na magurudumu yaliyomea kama nyota.

sisi kama vijana tulisema gari hili ni ya kuvutisha sana kuliko yote. Mimi na rafiki mwenzangu tuliona basi hii inapendeza mno hadi uso wa mwenzangu ulijawa na furaha kama kipofu aliyeona kwa mara kwanza maishani mwake.

Dereva wa basi hilo alikuwa akawa amekaa macho beruberu na nywele zake zilimtimika tim tim. Kitu moyoni mwangu ilisema nisingie kwa hilo basi lakini nilikuwa na chelewa kwenda kanisani.

Mimi na rafiki mwenzangu tuliingia kwa gari hili na gari iling’oa nanga kuelekea kanisani. Dereva huyu aliendesha gari kwa kasi sana . Alipoongeza kasi, roho yangu ulidunda du du du. Sisi maabiria tulitoa onyo kali kwa dereva apunguze kasi lakini wapi?. Hakutusikiliza kabla ya kufumba na kufumbua macho yangu, tuligongana na gari lingine na basi letu likapinduka.

Mguu wangu ulijawa na uchungu na nilitamani ardhi ipasuke inimeze. Niliokolewa na daktari na nikakimbizwa hospitali.Nililazwa hospitali na nikapewa habari sikuamini maishani mwangu. Rafiki yangu alikata kamba kwani damu uliisha mwilini.

Machozi yalinitoka kapa kapa na wazazi wangu hawakuamini pia habari hiyo. Ndio nilijifunza kwamba wahenga na wahenguzi hawakukosea waliposema ajali haina kinga.

Similar Posts

2 Comments

  1. This is good mnaheip upcoming generation kwa maarifa kupindukia. Kupitia kwenyu watakua na uwezo wa kuandika na hata kuwa na utunzg bora. Kazi njema. Ishaallah

Comments are closed.