Insha ya asiyekubali kushindwa si mshindani.
siku nilioongojea kwa hamu na ghamu ilifika. Niliamka asubuhi baada ya jimbwi kuwika. Nilienda bafuni kushtaki uashafu uchafu. Maji yalikuwa baridi shadidi.
Nilivaa nguo zangu nikinywa chai kwa mkate iliyokuwa tamu kama asali. Nilipomaliza, nilianza safari kwenda shuleni. Siku hiyo ilikuwa siku ya mwisho ya muhula wa kwanza. Nilipofika shuleni wazazi walikaribishwa na kuketi kwa viti vilivyokuwa nyeusi tititi.
Mzazi wangu aliofika, nilikuwa na furaha riboribo. Niliketi uwanjani na wanafunzi wenzangu kwa timu yetu nyekundu. Hiyo siku niliomba mwenezi mungu atupe usaidizi ili timu yetu iwe mshindi mwaka huu.
Nilingojea kwa udi na uvumba ili darasa letu liitwe mwanzo mwa uwanjani. Darasa letu ilipoitwa, nilichemka chem chem kuwa tayari kushinda mashindano ya kukimbia.
Tulipoanza kukimbia , nilikimbia kwa haraka sana kama swara aliyekimbizwa na simba. Timu yangu ya nyekundu ilinishangilia kwa kuwa wa kwanza kwa mashindano. Mwanafunzi moja wa darasa la nane aliyekuwa mweupe pe pe pe alikuwa mrefu kama mlingoti, alijaribu sana juu chini kunipita.
Tulpomaliza mashindano , huyu mwanaunzi alikuwa akisema kwamba yeye ni mshindi. Roho yangu ilikuwa na huzuni mno na karibu nikufe moyo.
kwa mshtuko, mwalimu mkuu aliniita na kunipea medali ya kuwa nilikuwa wa kwanza. Alisema alichunguza vile ambavyo nilikimbia. Nilikuwa na furaha sana na timu yangu kunisherehekea. Nilipogundua kuwa wahenga na wahenguzi hawakukosea kwamba asiyekubali kushindwa si mshindani lakini nilifurahi kuwa hatimaye niliibuka mshindi.