Insha ya asiyeskia la mkuu huvunjika guu.

EVERYTHING ON JUMIA
man in red polo shirt sitting near chalkboard
Photo by Andrea Piacquadio on Pexels.com

Niliamka asubuhi na maema baada ya jogoo kuwika. Nilienda bafuni kuogelea maji baridi shadidi. Nilipomaliza, nilienda kuvaa nguo zangu zilizonifurahisha sana. Nilienda sebuleni kuianywa chai kwa mikate iliyokuwa tamu kama asali.

Nilipomaliza, nilitoka nje nikiwa na furaha mpwitompwito hapa na pale kutafuta rafikia yangu wa kufa na kupona kucheza na yeye. Kumtafuta, hakupatikana. Ilibidi niende nikamtafute nyumbani mwao. Nilipomwuliza mzazi wake, alisema kwamba alitoka na marafiki zake.

Nilienda nyumbani kupumzika ningojee hadi saa tisa ili nitoke nikacheze na yeye. Nilingojea kwa hamu na ghamu saa kumi ifike ili nicheze na rafiki yangu. Ilipofika saa kumi nikatoka nje, kile nilicho ona kwa macho yangu sikuamini.

Niliona rafiki yangu akiivuta sigara akiranda randa na marafiki zake walivyokuwa na tabia mbovu sana. Walivaa suruali yao kama chupi ikionekana. Rafiki yangu juma alikuwa amepiga maji akiwa akitembea ovyoovyo na macho yake yalikuwa mekundu.

kwa haya yote nilijua kwamba anatumia dawa za kulevya. Nilienda kumuonya rafiki yangu juma kwamba dawa za kulevya ni hatari sana kwa binadamu na mwishowe atakata kamba. Nilipomwambia haya yote Lo! yale matusi makubwa aliyoniambia nilishtuka mno hata marafiki zake walinicheka kwa kwa kwa.

Nilikuwa na huzuni sana na machozi yalinitiririka tiritiriri nikijua kwamba maneno haya yote yalimpita kwa sikio hili yakatoka kwa sikio lile jingine. Ilibidi nipige ripoti kwa wazazi wake.

Wazazi wake waliposikiliza rafiki yangu juma aliadhibiwa na wazazi wake huku nikijua kwamba asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Kutoka siku hiyo sikutamani kuwa rafiki ya juma kwa hayo masahibu yaliyonisibu niliapa kuwa sitakuwa sahibu kwa juma tena.

Similar Posts