Insha ya barua na aina zake

Insha ya barua na aina zake. Ni maandishi yenye kutoka mtu mmoja hadi mwingine.
Zipo aina mbili.
1. Kirafiki au kindugu.
2. Rasmi.

Kirafiki au kindugu.
Ni baraka ambazo wenye uhusiano wa kirafiki au kindugu
huadikiana kwa lengo la kujuliana hali.
Muundo:
a. Anwani moja.
– Ni ya mwandishi na huandikwa upande wa kulia wa karatasi.
-Yaweza likaandikwa kwa mtindo wa wima au mshazari.
- Ikichukuwa mtindo wa wima aya zitaanzia mwanzoni na
- aya mpya kubainishwa kwa kuwacha mistari.
- Ikiwa ni mshazari aya itaanzia hatuwa chache kutoka pambizoni.
b. Tarehe.
– Huandikwa chini ya anwani ya mwandishi.
c. Mtajo au mwanzo.
– Anayeandikiwa hutajwa hapa.
Kwa sahibu
Kwa mpendwa.
d. Utangulizi.
– Ni salamu kwa anay andikiwa hutolewa hapa.
e. Mwili.
– Ndicho kiini cha barua kila hoja ijadiliwa katika aya yake.
f. Hitimisho.
– Mwandishi ahitimishe barua akionesha matarajio ya kukutana na anaye mwandikia barua.
g. Kimalizio.
– Wako mwaminifu – upande wa wima upande wa mshazari – wako mwaminifu.