insha ya barua rasmi

Insha ya barua rasmi.Huandikiwa kwa mtu usiyo na uhusiano naye wa kirafiki au wa kindugu. Ni za aina nyingi.

Aina za barua rasmi.

crop author writing in notebook with feather at retro table
Photo by furkanfdemir on Pexels.com

–         kuomba kazi

–         kuomba msahama.

–         Kutoa maoni.

–         Kuomba ajira.

–         Kuonga mfanyikazi.

–         Kutafuta kazi kutoa mwaliko.

–         Kujibu ombi la kazi.

–         Kulalawikiwa jambo fulani.

–         Kupongeza jambo fulani.

Lugha rasmi hutumika katika uandishi.

Muundo:

1.    Anwani ya mwandishi.

–         huandikiwa sehemu ya kulia ya karatasi, kama hutiwa 

mwishoni mwa kila mstari wa anwani na nukta hutiwa kwa

kila jina la jiji.

yaweza kundikiwa kwa mtindo wa wima au mshazari.

2.    Tarehe.

–         Huandikiwa chini mwa anwani ya mwandishi.

3.    Anwani ya mwandikiwa.

–         Huandikiwa sehemu ya kushoto chini ya tarehe, acha mstari mmoja baada ya kuandika.

4.    Mwanza au mtaja.

–         Uhusiano wa kikazi hudumishwa m.f kwa bwana/ bibi bwana/bi.

5.    Tanbihi.

–         Endapo ni barua kwa mhariri. Anza kwa mhariri.

6.    Kusudi au mada.

–         Huandikiwa chini ya mtajo. Kwa mfano mint/yah/kuh.

–         Kiini kiwe kifupiu na kinacho fumbata ujumbo wa barua kwa muhtasari.

–         Huandikiwa kwa herufi kubwa, na kisha kupigiwa mstari na kuna utangulizi.

7.Mwili.

Aya ya kwanza izungumzie kusudi la kuandika narua kwa muhtasari.

Aya zingine zizungumie kiini cha kuandika barua kwa kina kila hoja ijadiliwe na kukamilika kwenye aya.

8.Hitimisho.

Hitimisho mawazo yako hapa kwa kuonyesha maoni yake kuhusu jambo ulilokuwa unajadili.

9. Kimalizio.

Uhusiano kuhusu mwandishi na mwandikiwa uzingatiwe. Mf: wako mwaminifu.

Tanbihi.

1.    Iwapo mtindo wa wima ilitumiwa, kimalizio huwa upande wa kushoto pembezoni.

2.    Ikiwa mtindo ni wa mshazari kimalizio huamdikwa upande wa kulia.

3.    Sahihi hutiwa chini ya wako mwaminifu.

4.    Jina huandikwa chini ya jina iwapo ni ya kuomba kazi.

5.    Cheo kinaweza kuandikwa au kisiandikwe.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts