Insha ya barua ya kirafiki

Barua ya kirafiki.

Middemb LTD,

S.L.P 12134,  

Nairobi.

1/03/2023.

Kwa mzazi ( Baba)

Je uhali gani? Pokea salamu kemkem kutoka kwa familia yako. Wote wanatumai u  buheri wa afya. Sisi hapa nyumbani tu wazima kama kigogo. Kila mmoja ana hamu ya kukuona lakini uko mbali na sisi kwa hivyo hilo haliwezekani hata. Natumai unaendelea vyema huku tukikuombea kwa mola akujalie wakati mwema huko kuliko. Natumai pia kazi yako yaendelea vyema.

beige envelopes with triangular seal flap
Photo by Diana Akhmetianova on Pexels.com

Sababu ya kukuandikia barua hii ni kukujulisha jinsi mambo yalivyo humu nyumbani. Sisi tunaendelea vyema bila kasoro yeyote ile huku rabana akitumiminia baraka zake za kufana. Chimbuko zilizoko ni kidogo tu ambazo hata hivyo haziwezi kuegemea pande yoyote ile ya familia yako. Maswala ninayo ya kukusulisha ni machache tu.

Wiki iliyopita mama aliweza kuugua. Huo ulibadilika kuwa mgumu sana lakini kwa mapenzi ya mola aliweza kupona. Jambo hili liliweza kukera wana wako. Sasa twamshukuru mola kwa kumjalia hali hiyo ya fanaka.

Msimu uliopita tuliweza kaupata mazao chunguzima shambani na hata katika mifungo uliyoacha. Ng’ombe kadhaa wameweza kujifungua huku wengine wakizaa mapacha. Mvua iliweza kunyesha vizuri sana huku mafuriko yakionekana humu nchini.

Hiyo inaonyesha kuwa mola hawaachi wana wake. Katika masomo, wana wako pia hawaachwi nyuma kwani kila mmoja anatia bidii za mchwa kuhakikisha amefaulu zaidi. Matumaini yetu ni kuwa na maisha ya starehe siku zisazo kwani elimu ndiyo mwangaza siku hizi.Nafahamu ujuavyo, kaka kuwa aliweza kupandishwa cheo katika kampuni ya ‘ Telcom’. Jambo hili linadhihirisha kuwa anaonekana kuwa shupavu na mwenye bidii katika kazi yake.

Dada naye aliyekuwa akifanya kazi ya wazigi aliweza kujiunga ya chuo kikuu cha Nairobi mwezi uliopita. Alionelea ni vyema kuendelea na masomo yake kwa manufaa ya siku za usoni.

Familia yako imeweza kupata sita kemkem kutoka kwa wanakijiji kwa jitihada zao zinazoashilia umoja na umakinifu. Ninayofuraha kukushiria kuwa nitafanya bora zaidi iwapo jitihada zako zitakuwa za kufana. Ninayo humu ya kufanya shule na hata kiria chetu kiwe na maarifa zaidi.

Nina matumaini makuu na ya kufana kuwa utaweza kupata habari hii nilivyoandika na ufafanulizi wake zaidi. Naomba mola akubariki na akusalie hali njema.

Wako mwaminifu

___

jina.

Similar Posts