Insha ya churuchuru si ndondondo.

Naam ukweli usemwe. Heri kupata kidogo kidogo kila siku kuliko kingi siku moja. katika kitongoji cha amani paliondokea mzee moja aliyekuwa na wana wawili. Wanahao walimsumbua kila kucha kuwa walitaka mali yao.

mzee huyo hakusita kuwapa. Baada ya kukabidhiwa mali yao waliuza na kutorokea mjini ambapo walijitoma katika anasa za dunia. Maghulamu hao walipenda raha huku bila kumbuka mzazi wao.

Kasiki moja kijana aliyekua kifungua mimba alipatwa na hitaji la ghafla. Hakuwa na mbele wala te, alipata msaada kutoka kwa rafikiye ambapo alimuahidi angerudisha baada ya miezi miwili.

Alihitimisha hitaji lake na akapata kazi. Mshara wake aliutumia kiholela holela bila ya hata kukumbuka babaye. Kijana huyu akiujiendeleza. Shida ilimwandamana ingawa alifanya kazi madeni haya hayangesemeka.

Baada ya miezi miwili kukamilika rafikiye alimwendea na kuhitaji hela zake. kijana yule alimharifu kuwa angepata hela baada ya majuma mawili. Sahibu alidubiri adi majuma yake kamilikia. Aliporejea lijana yule alimfahamisha kuwa akuwa amepata.

Rafikiye alimshika na kumpeleka kwenye kituo cha polisi. Alijuta huku akisema heri kidogo cha kila siku kuliko kingi cha siku moja. Baba yake alilipa deni hiyo hatimaye akawachiliwa huru.

Similar Posts