Insha ya haba na haba hujaza kibaba.

EVERYTHING ON JUMIA

Nilipokuwa mtoto mdogo, nilitaka kuwa na kazi nzuri kwani shuleni nilikuwa na soma vizuri shuke ya upili nilikuwa na rafiki wa kufa kuzikana tulipokuwa tunapendana kama chanda na pete.

cute rabbit with eyeglasses
Photo by Anna Shvets on Pexels.com

Kitu alichonacho na mimi sina tulikuwa tunasaidana. Tulitaka tumalize katika kidato cha nne ilituwe na kazi nzuri na tuwe tumefaulu. Tulipomaliza kidato cha nne, sikuwa kazi chochote.

Rafiki yangu wa kufa kuzikana, hapo ndio alinigeukia kigeugeu na hata hakuwa akinisaidia tena. Niliachwa maskini hohehahe na kulala kando ya barabara. Hizo siku nilikuwa na huzuni sana.

Kila siku nilikuwa na jikaza kisabuni na kupata pesa kidogo sana ya kununua chakula. kila siku niliomba mwenyezi mungu anisaidie na kweli nilisaidika sana.

Nilinunua pikipiki na kupeleka abiria mahali anapotaka. Nilipopata pesa, niliweka kwa benki kwa kuwa haba na haba hujaza kibaba. Nilifurahi sana na kwa kweli kila wiki marafiki zangu walikuwa wakini chekelea.

Miaka mitano zilizopita, bado walikuwa wananitusi bado. Nilikuwa na rafiki mwingine anayeitwa Ian. Alinisaidia sana na kwa kweli alikuwa tajiri sana.

Alinipea kazi nyingine muhimu sana. Kazi hii ilinipa pesa nzuri. Nilipokuwa nyumbani pangu, wezi watatu walinivamia . Nilipowaona nyuso zao, hawa wezi sikuamini. Lo! rafiki aliyekua shule yangu ya upili ni mwizi.

Walinipiga na kunigonga na kila kitu. Mra si kitabu, sufuria, mshipi, viatu, kikombe yani karibu kila kitu kwa nyumba.

walipokimbia walinitoroka na vitu vyangu lakini si zote. Hawakujua kuwa jirani yangu ni polisi. Alinisaidia sana kuwashika. Walposhikwa walipelekwa gerezani na vitu vyangu havikupatikana. Sijawahi kuona adui mbaya kama ule rafiki yangu. Huzuni ilitanda moyoni mwangu. Hata hivyo, niliamua kujkaza na kuendelea na maisha kwani ilandikwalo haifutiki.

Similar Posts