Insha ya harusi

Insha ya harusi.



Tuliamka alfajiri yamajogoo tayari kwa safari tuliyoingojea kwa siku nyingi. Tulijitayarisha kwa haraka ili tusichelewe kuenda kumlaki dada yangu katika eneo la harusi katika mbio mbio za sakafuni, tulipatana na wenzetu njiani, tulichukua gari na kuondoka. Tulikuwa karibu kuwasili eneo la harusi yenye ilikuwa katika kanisa la shauri moyo Adventist church ambayo ilikuwa la wana sabato. Tuliwasili na waalikwa wengine kumeza punje, maarusi wali wasili kanisani.


Mwenye aliongoza dini aliwasili piga kuongoza sherehe hilo, harusi ilianza hatimaye, watu kuimba kwa shangwe na vigelegele kuona harusi kama hiyo. Dada yangu alifurahia kuona watu walisadia katika kupamba harusi hii na kutiririka kwa machozi.



Walimsaidia sana, masaa ya kuvishana pete ilifika, ahadi na miadi zikatolewa na kuwa bwana harusi na bibi harusi walikuwa bibi na bwana. “ Shangwe na vigelegele.” Nilisema kwa furaha, bismilai zilipigwa, watu walikuwa na haraka ya kukula sasa, maarusi walienda kupiga picha na watoto wazururaji.



Watu walielekea kwenye sehemu ya pili, mahali pazuri pakumpumzika na kukula na kunywa, ilikuwa kukata na shoka, waarusi walifika na watu walicheza kama daudi. Bwana na bibi harusi walikata keki na watu wakala.



Kwa harusi walipokea zawadi kutoka kwa waalikwa. Maarusi kuelekea kwa fungate ,watu walifurahia kama ndama. Watu walifumukana. Maarusi na waalikwa kutengea watoto wa mitaani na mayatima chakula chote na keki. Sitawaisahau hii siku ya kukata na shoka.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts

One Comment

Comments are closed.