Insha ya kifo hakina huruma hata chembe.

EVERYTHING ON JUMIA

Mfano wa insha ya methali.Itakayosaidia wewe katika mtihani au masomo.

person holding gray twist pen and white printer paper on brown wooden table
Photo by Cytonn Photography on Pexels.com

Mfano wa insha ya methali ifuatayo .Below is an example or mfano wa insha ya methali: Anza kwa wingu kubwa jeusi lilitokea upande wa mashariki, baadaye matone mazito mazito.

KIFO HAKINA HURUMA HATA CHEMBE.

Yalianza kunyesha. Ngurumo za radi zilihinika angani. Watoto walijawa na woga wa shumdwa. Fuadi wangu ulinidwikadwika mithili ya tokomire za wazaramo.Mvua yenyewe ilinyesha kwa fujo. Upepo mkali ulizing’oa paa za nyumba . Tulikaa kimya na kutulia kama maji mutungini tusijue la kufanya . cha mbilecho wamantiki na wananatiki wenye lisani za utaalamu na utalamidhi “ Jambo lisilolijua ni usiku wa giza.

Baada ya mwia wa kelbu kuukalia mkia, maji yalikuwa yamefurika furifuri na kuingia vyumbani vyetu.Nilishikwa na huzuni kama mja aliyehukumiwa kunyonga, na sasa yuaongozwa katika kijia chenye giza, na hajui mambo yatakavyokuwa baada ya nukta chache.

Nilikuwa na wazazi wenye fulusi lukuki. Walinifunza na kunienzi kama mboni za maozi yao. Niliishi  maisha ya taha mustarehe bimithili ya sultan bin jerehe.Sasa msli yetu yote yangesombwa na maji.Tulikimmbia  ili kuyaokoa maisha yetu. Mauti yalikuwa yakitukodolea maozi. Wengine walibaki nyuma wakisema eti wao ni stadi wa kuogolea.Nasi tulikimbia kwani wahenga na wahenguzi wa jaai na jadudi hawakumlazimisha kiwete kuparanga mti waliponadi, “ Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.

Katika harakati zetu hizo, tulikutana na asaeli wawili. Nilitetemeka bimithili ya kifaranga mwenyw manyoya haba  wakati wa kipupwe tulipambana na hayawani hawa wawili na baadaye tukawashinda. Kwani wahenga waligunga ndipo waliponadi, “ Asiyeshindwa si mshindani.”

Kwa bahati mbaya maji yaliongezeka na tukasombwa sisi sote. Hapa kila mtu alitumia ugwiji wake ili kuyanusuru maisha yake.Nilipiga bismillahi kula rabimsta ili anipe uwezo wa kuepukana na mauko haya, Baada ya muda wa tembe kumeza punje la mahindi, nilikuwa nchi kavu. Nilimshukuru rabuka huku nikitumai ya kuwa mungu si mfaki.

Kapu langu lilikuwa tupu na nilihitaji maankuli.Ghafla bin vuu niliskia mgurumo wa magari. Loh! Niliona magari yaliyochorwa mslaba mwekundu, nami nilikuwa nimejilaza ardhini kwani nilikuwa nimechoka. Hoi bin tiki tamthili ya punda wa dobi.Niliamka na kujikakamua hadi magari yaliyopita  habla.

Walitoka kwenye gari huku wamevaa nguo za kupiga mbizi.Walinipea chakula nami nikala kwa ulafi kama majuniu wa majunju.Manusura waliokolewa na wengine wakapelekwa hospitalini. Tulipewa nguo, chakula na mabalanketi .Tuliwasifu kwa wema wao kwani. “chanda chema huvikwa pete.”

Baadaye, waliopatwa na mauko walipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Mimi mwenyewe niligundua ya kuwa nilikuwa nimepiwa na wavyele wote wawili. Nililia kwi kwi kwi. Sikujua nianzie wapi na nimalizie wapi. Mawazo kochokocho yalinizunguka kichwani mwangu.

Wingu la jitimai lilitanda miongoni mwitu. Baadaye nilipelekwa kwa mbiomba wangu. Ndipo nilipoamini ya kuwa kifo hakina huruma hata chembe.

Similar Posts