Insha ya kumbukumbu Muundo wake ( step by step)

Insha ya kumbukumbu Muundo wake ( Step by step).Ni taarifa zilizorekodiwa kuhusu mambo muhimu yaloyozumgumziwa katika mkutano rasmi mwa sajili ya kumbukwa au kurejelewa.

smooth round colorful shapes with wavy edges
Photo by Chris F on Pexels.com

Muundo una kumbukumbu.

Kumbukumbu huwa mkutano wakipekee yenye:

1.Kichwa 

Kichwa cha kumbukumbu hutaja wanaokutana, aina y mkutano mahali pa mkutano pamoja na tarehe na saa ya kufungika kwa mkutano wenyewe.

–         Kichwa huandikwa kwa herufi kubwa mfano: KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA KAMATI 16/04/2019 SAA NANE KAMILI KATIKA LIKUMBI WA SHULE.

2. Utangulizi

Sehemu hii huangazia ushirika wa wanachama katika mkutano.Kwa kawaida kwa wahudhuria.

a.     Waliohudhuria.

Majina ya waliohudhuria hurodhesha uwa mpangilio maalum kwa kuanza na mwenyeketi akifuatwa na naibu mwenyekiti na wengine wenye vyeo katika kamati hiyo.

b.     Waliotumia hudhuru kwa kutohudhuria.

Majina ya mwneyechama ambao kwasababu fulani walikosa kuhudhuria mkutano lakini waliomba ruhusa.

c.     Waliokosa kutuma hudhuru kwa kutohudhuria.

d.     Orodha ya waliokuwa ikiwa wako.

3.    Agenda ya mkutano.

Ni mambo yaliyopangiwa mujadi;

1 maelezeo kutoka kwa mweneyekiti.

2. Kusoma na kudhitibitisha kwa mkutano uliopita.

3. Rekodi ya mkutano wa sasa na maaumizi ya maswala makuu ya agenda.

4. Shughuli nynginezo.

– huwa ni masuala ambayo hayakurodhesha kwenye agenda kuhaliziia kwa mkutano kwa mambo.

4.    Nafasi ya kutiwa sahihi ya mwenye kiti na katibu pamoja na tarehe izo.

–         Sabihi hutiwa kwa mkutano utaofuata baada ya kusoma kwa kudhibitisha kwa mkutano huo kuwa ni sahihi.

Sifa za kumbukumbu.

–         Unapoandika kumbukumbu ni muhimu uhakikishe sifa zifuatazo zinazotokea.

1.    Mambo yaandikayo ni rasmi. – Kwa hivyo yaandikwe kwa muundo na mtindo rasmi.

2.    Mambo huandikwa k.m mkato – Hata kichwa huandikwa kwa ufupi ili kurejelew haraka.

3.    Yaandikwayo ni muhtasari – wa majadiliano na maamuzi ya kundi na sio ya mwanachama binafsi.

4.    Mambo huandikwa kwa nafsi ya tatu na kwa usemi wa taarifa. – wakati hutumiwao ni ule uliopita.

5.    Majina ya wanaotoa mchango hayandikwi isipokuwa tu panapohitajika watu wa kutekeleza mambo fulani.

6.    Huzingatia uakifishaji – mfano herufi kubwa kuandika kichwa, tarakimu kuakifisha agenda.

7.    Hutumia latilahi maalum  kama vile: Lishauriwa, iliandikwa, ilipendekezwa, ilikubaliwa.

Umuhimu wa kumbukumbu ( importance ).

Katika ulimwengu wa sasa mikutano hii muhimu na hufanywa mara kwa mara – kila mkutano rasmi unapofanya kumbukumbu huandikwa kwa ajali ya kuwakumbusha wahusika yaliyozungumziwa hufuatilia utekelaji wa yaliyo afikiwa.

Mfano:

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA WANACHAMA CHA KISWAHILI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA SHULE YA UFANISI, TAREHE 10 JANUARI 2014 KUANZIA SAA TISA ALASIRI.

Walioudhuria.

Paulo maket – mwenyekiti.

Mariamu zuberi – katibu.

Jepkorir jonui – Mbazihi.

Kasidi Obiera – Mwanachama.

Nyachama Ondieki – Mwanachama.

Johson brown – Mwanachama.

Stacey banks – Mwanachama.

Aliyetuma udhuru.

Wagechi mugo – mwanachama.

Aliyekosa kuhudhuria.

Abdulahi Binda – mwanachama.

Mwalikwa.

Bi Risper Mwasa – mlezi wa chama.

Agenda.

1.    kufunguliwa kwa mkutano.

2.    Kusoma na kudhibitisha kwa kumbukumbu zaawali.

3.    Masuala ibuka kutokana na kumbukumbu hizo.

4.    Kuzidisha idadi ya wanachama.

5.    Kuandaa makongamano.

6.    Kuwafunza wanafunzi.

7.    Masuala mengineyo

8.    Kufunga mkutano.

kuna mifano ingine ya kumbukumbu ambao unaweza tumia kuthibitisha kwa kuandika insha ya kumbukumbu. Chini yako kuna insha ya kumbukumbu kamili ambao umeandikwa na mwanafunzi katika shule ya upili kidato cha tatu.

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA WALIMU WA KISWAHILI ULIOFANYIKA KATIKA OFISI YA MKUU WA IDARA TAREHE 22/2/2022.

WALIOHUDHURIA.

 1. Yakobo juma – Mwenyekiti.
 2. Hamidi hamisi – Katibu.
 3. Aisha Juma – Mhazini.
 4. Fatuma Ali
 5. Yusufu Abdi.
 6. Jabali Kipchumba.
 7. Amina mawazo.
 8. Sudi Maria.
 9. Tunu naomi.

WALIOTUMA UDHURU.

 1. Mariamu Maria.
 2. Elimu banda.
 3. Hasidi kantai.

WALIOKOSA KUHUDHURIA WALA HAWAKUTUMA UDHURU.

 1. Annah kigosi.
 2. Kabasi mawazo.

AJENDA ZA MKUTANO.

 1. Kufungua mkutano.
 2. kusoma na kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.
 3. Masuala yaliyozuka kutokana na kumbukumbu za mkuatno uliopita.
 4. okosefu wa vitabu vya kusoma na kudurusu.
 5. Maandalizi ya kudhuria jumba la sinema kwa ajili ya kuvitazama vitabu vya tamthilia.
 6. shughuli za ziada.

KUFUNGUA MKUTANO.

Mkutano ulifunguliwa saa nane adhuhuri kwa maombi yaliyongozwa ya yusufu abdi. Mwenye kiti aliwakaribisha wanachama na kusisistiza juu ya umuhimu wa mkutano huo.

Kumb: 2/2/2022

kusoma na kuthibitisha.

Katibu wa tume aliwaongoza wanachama kuzisoma kumbukumbu. Baaada ya kuzisoma aliungwa kono na Jabali kipchumba kupendekezwa na Fatuma Ali, Mwenyekiti na katibu walizitia sahihi na kudhibitisha kuwa zilikuwa tu kamilifu.

Kumb: 3/2/2022

Masuala yaliyozuka kutokana na kumbukumbu za mkutano uliopita.

Kutokana na kumb 2/1/2022 iliyohusu mipangilio ya mitihani wa kiswahili utakao fanywa na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne. Mitihani Ilitayarishwa na kuchapishwa.

Kumb 7/1/2022 iliyohusu hazina ya kandalizi wa mashindano ya kiswahili kati ya shule zilizokaribuna yetu.

Kumb: 4/2/2020:

ukosefu wa vitabu vya kusoma na kudurusu.

wanachama walishauriana kwamba ni vyema kuwanunulia wanafunzi vitabu vya kusoma na vya kudurusu ili kuwa bora na wabombee katika kiswahili. Walianzisha mchango Ili waweze kupata hela ya kuvinunua vitabu hivyo.

Kumb 5/2/2022

Maandili ya kudhuria jumba la sinema kwa ajini ya kuvitazama vitabu vya tamthilia.

wanachama walikubaliana mipango ya kuwapeleka wanafunzi kuvitazama vitabu vya tamthilia ili waweze kupata kuvielewa kwa kina zaidi. Walijadiliana kuhusu njia wa takayo tumia kusafiri na pia vyombo vya usafiri na jinsi ya kuwafunza wanafunzi wao.

Kumb:6/2/2022

Shughuli za ziada.

wanachama walionelea ni vyema kuendelea na mikutano mingine na kuwasaidia wanafunzi na kuwaelekeza katika masomo yao. Amina mawazo aliwahimiza wanachama kujiita nguvu na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuwaelimisha wanafunzi.

Kufunga mikutano.

Pasi na masuala mengine ya kujadili. Mwenyekiti aliufunga mkutano takriban saa kumi unusu alasiri Aliwashukuru wanachama kwa ajili ya kujitokeza. Tuna neema aliufunga mkutano kwa maombi.

Thibitisho.

Mwenyekiti_________________ sahihi____________ Tarehe.____________

Mwenyekiti_________________sahihi ____________Tarehe.______________

Similar Posts