Insha ya likizo yangu.

Ilikuwa mwezi wa oktoba karibu tufunge shuleni kwani ilikuwa muhula wa mwsiho tufanye mtihani na kuelekea darasa lifatao katika mwaka ijayo. Niliketi sebuleni nikiskiza wazazi wangu wakipanga likizo ya kwenda kuona Bibi na Babu yangu mashambani.

Likizo hili lilipangwa iwe mwezi wa Novemba. Baba na mama walinialisha niwe nikijitayarisha niwe tayari kuenda likizo huu. Ilikuw mara yangu ya kwanza kunda Likizo kama hii kuona Mababu wangu tangu niwe mtotoni.
Siku zilipita kwa mwendo wa aste aste, hapa fikra za likizo ilinibingira akilini nilitamani ardhi ipanue ifungue inimeze kwa siku hio itafika nini?. Niliskia kwamba kwa mababu yangu ni pazuri. Kuna bwawa la kuogelea, wananyumba kubwa na hewa ya huko ni safi mno kuliko hii hewa ya Nairobi iliyochanganishwa. Yani hewa si safi vile.
Kwa siku niliyongojea kwa hamu na ghamu ilifika. Siku huu niliamka asubuhi na mapema baada ya jogoo kuwika. Niliogelea maji ina joto lakini si sana. Nilichukuwa muda kiasi, nikaskia mlango wa bafu ukigongwa kama ndege anayedonoa sisimizi. ” fanya haraka.” Niliskia sauti.
Kutoka kwa bafu, nilivalia nguo yaliyonipendeza nikawa nimejawa na furaha. Nilishuka ngazi kuelekea sebuleni kukaa kwenye kochi moja. Mimi na familia wenzangu tulichukuwa kiamsha kinywa hapa harufu ya mayai na soseji yalitufanya tuwe na tamaa na ilikuwa tamu mno kama asali.
Tulipomaliza, tuliweka mifuka na sanduku zetu nyuma ya gari, tukijitayarisha kuanza safari. Ghafla bin vuu, tulingoa nanga kuanza safari yetu kuelekea mashambani. Kwa dirisha niliona vitu vingi. Magorofa, magari mengi, miti yakipita kwa kasi, wamyama pori, na kadhalika.
Baba alikuwa anatuelezea vile barabara za leo zimebadilika akitafautisha na za kale. ” tulikuwa tunaenda safari moja kwa siku mbili kwa barabara haya yalikuwa bovu. Watu walikuwa wakisafiri kwa siku miwili inabidi ulale usiku kwa gari na siku ijao unaendelea na safari, lakini siku hizi ni nywe.” Baba alisema na kuendelea. ” Unaona magorofs hsys, hayakuwa hapa, hapa ilikuwa kichaka na watu walikuwa wachache.”
Ala! kwa haya yote baba anasema ni kweli?. Nilikuwa wapi haya yote yakiwa yamefanyika sikuwa kwa dunia bali kwa tumbo la mama. Maelezo za kale kutoka kwa wazazi wangu ili shangaza sana. Safari ilikuwa ndefu mno, hivo ndi nilihisi, nilichoka na lupiga mayowe nikapatwa na lepe ya usingizi nikalala, kisha nipate nguvu badae nikiamka.
Nilipoamka, Lo! tulishafika. Mbele yetu ilikuwa langu kubwa ukifunguliwa na mlinzi. Tulingia ndani polepole na kukaribishwa na wajakazi. Nyumba ilikuwa kubwa na mazingira yalikuwa ya kuvutia, Tulipo karibishwa ndani ya nyumba niliwaona Bibi na babu yangu wakinikaribisha. Walinikukumbatia na kunikaribisha wakiwa na furaha mpwito mpwito. Nilionyeshwa bwawa la kuogelea, ilikuwa kubwa na kwa kweli niliogelea na ilinimpendeza. Kwa siku hilo sitawahi sahau.