insha ya maisha yangu.
Nilizaliwa kijijini kazana na wazazi wangu Bwana na Bi mkinga. Waja wengi hapendi kutaja umri wao, labda wasiitwe wazee, ila mimi sina haja ya kuuficha umri wangu. Hata nikitaka kuficha mkunyazi usoni yatani saliti yeyote anijuaye sasa anajua nimefika umri mpevu wa miaka zaidi ya themanini. Namshukuru jalia kwa kunijalia miaka sabini ya wastani wa kuishi mja na wangu wa juu. sio kwamba najitopa lakini labda umri wangu wa juu wadhihirisha kuwa nilidumisha mbele hasa kuwa heshimu wavyele wangu. Naye mterehemezi akanijalia maisha marefu.
Kikwetu, sasa nimefikia umri wa kumtolea mungu dhahinu na nina mshukuru kwa hili na mengine. Ingawa mwana mtamba kule humpita mzee wa kale naamini mimi ni miongoni mwa watu wachache wanaoishi mimi ni miongoni mwa watu wachache wanaoishi waliowahi kuiona historia kamili ya nchi yetu na wanaoweza kukitambia kizazi cha sasa yaliyojiri. Nilikuwako enzi za wakoloni nikashiriki kando ya ukombozi na kumfukuza mkoloni. Nina ya kusema pia kuhusu hali iliyo leo hii ni mojawapo ya sababu za kutoka kuyaandika machache kuhusu miaka yangu.
Msemapo kuna uhuru nilizeni mie maana ya uhuru kwakua namjua beberu tangu kutawala kwake na jinsi tulivyomjua na hata alivyoyomea kwao baina ya 1958 – 1962 nilikuwa kiongozi wa krikasi kilichoitwa danger. Wenzangu walinita kumbwewe kwa vile nilivyo jua kutumia leo lwa ustadi uli umtetemesha mzungu na bunduki yake. Niliwagwiza wengi kwa silaha yangu hiyo madhubuti.
Baada ya kunyakua uhuru nilikuwa na nafasi ya kunyakua gunda katika miaka sitini lakini nilidinda nikasema kuwa tulipigania uhuru ili tuwe na usawa wengui waliniona juha ila nikawaambia moyo safi ni bora kuliko fedha na dhahibu. Niliona wengi wakinyakua hivi na vile jambo lilanitetea matata kutoka kwa wale niliojaribu kuunya dhidi ya mambo hayo ajabu, nikuwa ingawa walinyakua vingi kufikia leo hakuna hata moja aliye hai.
Maisha yangu ni safi na vichahce nilivyonayo nimevifuka jasho. katika umri wangu wa makamo nilifanya kazi katika ofisi nyingi za umma. lakini kazi niliyoipenda kuliko zote ilikuwa ya ualimu niliyoifanya kwa miaka ishirini. Kinachouridhisha moyo wangu nikwamaba niliwaona wengi wakipita kwa shani kupitia mkononi wangu. Sasa hivi kuna wengi walio wakumbwa katika ofisi kuu za umma ni fahari yangu kuwa walipita mikononi mwangu.
Kuishi kwingi ni kuona mengi, nami nimeyaona nikaya shiriki naye yakani komaza labda kwa kuwa mimi ni mwanambee nimepata heshima ya ndugu zangu hasa babangu marehemu aende asikarudi. Nimechukuwa wadhifa wa kuiongoza aila yetu katika shiughuli za kikwetu. Marehemu mamangu aliyemfuata babangu pia alinibahi kunishauri kabla ya kufanya lolote katika jamii yetu.
Tangu nilipostaafu kutoka ofisi za umma nimekua mshauri waviongozi, watumishi wa umma na hata wafanyibiashara. Wengi huja kupata ushauri wa namna ya kuishi na ala zao sio kwamba mimi ni mjuzi lakini labda niliyoyaona aushini mwangu yanawapa wengi mwelekeo tena mimi ni mkulima. Nahakikisha nayatia kitone cha mwisho nikipumzika baada kazi ya kipogoa mimea kushiriki nao. Ya leo nimetekeleza kesho ni ya mungu.
