Insha ya masimulizi – Hadithi ya Mafuriko.


Ilikuwa asubuhi ya jua kali na anga lilikuwa wazi kabisa. Kijiji kidogo kilichopitiwa na mto mrefu kilikuwa kimejaa shughuli za kawaida za kila siku. Watu walikuwa wakifanya kazi shambani, watoto walikuwa wakicheza kwenye mito midogo, na wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sokoni.
Lakini ghafla bin vuu, mawingu yalianza kujisanya angani. Upepo ukawa mkali mno na maji ya mto yakawa yanapanda kwa kasi. Kulikuwa na dalili zisizotarajiwa za mafuriko yajayo. Watu walianza kutambua hatari na hofu itakayotawala katikia mjini yao.
Vilio vya tahadhari vilitangazwa kupitia spika kubwa zilizokuwa zimeenezwa katika kila pembe ya kijiji. Watu waliharakisha kuhama kutoka maeneo ya chini na kusaka makazi salama zaidi. Nyumba zilifungwa haraka, na watu walijaribu kuokoa mali zao muhimu kabla ya maji kufurika.
Mafuriko hayo yalifika kwa kasi na ghafla. Mto ulijaa na maji yalifurika furifuri barabarani, hapa mashamba yalizamishwa na miti iliangushwa kwa nguvu ya maji. Watu walikimbia kwenye maeneo ya juu zaidi kama milima na nyumba za majirani.
Kijiji kilijawa na kilio cha hofu. Watu walipoteza kila kitu walichokuwa nacho kwa miaka mingi. Nyumba zilizokuwa nguzo za matumaini zilisombwa na maji, na mazao yote yaliharibiwa. Familia zilikuwa zimevunjika moyo na kukata tamaa wakijaribu kusaidiana na kuokoa maisha yao.
Watu waliweka juhudi za pamoja kukabiliana na janga hilo. Walitengeneza mitambo ya kusaidia maji kutoka ndani ya nyumba zilizozama na kuanza kujenga madaraja na barabara mpya baada ya mafuriko kupita. Pia, walitoa msaada kwa wale ambao walikuwa wamepoteza makazi yao na kuwaacha bila chochote.
Baada ya siku kadhaa za kazi ngumu, maji yalianza kupungua na maisha yalianza kuwarejea watu. Ingawa walikuwa wamepoteza vitu vingi muhimu, walijifunza thamani ya mshikamano na msaada wa kibinadamu. Kijiji kilijengwa upya nyumba zao na watu wakaanza kulima mashamba yao upya.
Kwa muda mrefu baadaye, hadithi ya mafuriko ikawa kumbukumbu ya changamoto kubwa na baadae ikawa kurasa mpya ya maisha kwa walw waliopitia hofu kama hili.