Insha ya memo
Insha ya memo. memo ni mkata wa neno memoranda lenye maana ya maandiko ya kukumbusha habari. Memo ni barua fupi rasmi ambayo hutumiwa katika mawasiliano baina ya watu mbalimbali hasa wafanyikazi mbalimbali kuwasababu kama vile:
1. Kuwakumbusha watu wajibu.
2. Kuarifu.
3. Kufahamisha sera.
4. kuweka kumbukumbu ya mambo na kadhalika.
Muundo wa memo.
1. Huandikwa katika karatasi maalum lenye anwani na jina husika.
2. Chini ya jina huandikwa jina memo kwa herufi kubwa kukolezwa rangi au kipigiwa mstari.
3. Upande wa kushoto chini ya mistari huandikwa tarehe.
4. Chini ya tarehe hutokezwa kumbukumbu ambayo hurejelea nambari ya barua hiyo.
5. chini ya tarehe huwa maelezo ya memo itatowa wapi – hapa cheo cha mtu huandikwa na chini yake maelezo ya memo inaenda kwa nani.
– Cheo pia hutolewa iwapo memo inapitia kwa mtu mwingine.
– Memo pia inaweza kuwa ina makala inatolewa kwa watu wengine.
– Chini ya hayo shabaha ya memo huandikwa kwa hati kubwa na kukolezwa wino au kupigiwa mistari.
– Mwili wa memo hufuata ukiwa na utangulizi mwedelezo na hitimisho.
– Chini yake hutokea sahihi ya mwandishi ikifuatwa na jina lako na cheo iwapo iko.
Mfano:
KlABU YA MAZINGIRA SAFI
SHULE YA UPILI YA MILII
MEMO
Tarehe: 11/1/2014.
Kumb: Manzi/cha/113.
Kutoka:mwenyekiti.
Kwa: mwalimu mkuu.
Kupitia kwa: mdhamini.
Nakala kwa: mwalimu mkuu shule ya upili ya ustawi mei ya wa manispaa.
KUH: USAFISHAJI WA MJI.
Kwa niaba ya mazingira safi humu shuleni ningependa kuumba idhini ya kushiriki katika shughuli za kutakasa mji hapo jumamosi tarehe 15-2-2014 wanachama hawa watashirikiana na wenzio wa shule ya upili ya ustawi pamoja na madiwani wa mji wa umma shughuli hii itaongozwa na masthiki moja wa mji.
Uambatano na wito wa kiabu hii tungependa mbio kwa umma na wakaazi wa mji huu, kuwa pana haja ya kuyawika mazingira yetu safi juhudi zetu zimetambuliwa na mstahiki moja. Hiyo ndiyo sababu alikomba kupitia kwako kushiriki katika shughuli hii.
Wanachama wataondoka shuleni saa tatu asubuhi na kuundi saa kumi jioni.
Sahihi
Nadhifa Tahara.
Mwenyekiti wa klabu.