Insha ya mgagaa na upwa hali wali mkavu.
Ukiwa na bidii za mchwa mungu hawezi kosa kubariki kwa yale kazi unaofanya. ” hadithi, hadithi ?.” mzee nazim aliuliza. Tukajaibu ” hadithi njoo.” Mzee Azim amekuwa mzee wa mali na pia wa heshima.
sisi kama watoto tulimtambua kwa yale amefanya na ikanipa nguvu nianze kufanya bidii maishani ili niwe kama yeye. Alijulikana jijini letu la tajira. Aliambiwa ajaribu siasa lakini alikataa kata kata.
Mzee Azim amesaidia sana jamii yetu, kulipia watoto wa shule karo, kupea vijana kazi na kusaidia familia yasiyojiweza kupata matakwa zao. Mimi ambaye mtoto mdogo hivi nilitamani kuwa kama yeye.
Tuliketi chini ya miti, pamoja na mzee Azim, kusikiliza kimya hadithi yake fupi ya maisha yake. Nilikuwa tayari kusikia kwa makini kwa maneno zake yanipe nguvu yakuwa kile nilichotaka kuwa.
“Nilipata pesa kidogo la kuanzisha biashara wa kuuza mkate, Wateja walianza kuja kidogo kidogo kwa muda wakawa kwa wingi. Kazi hili Ilinipa moyo wa kuendelea kazi hili.
wateja wengine waliniuliza kama naweza pelekea mikate hii kwa milangoni mwao. Sikukataa, kwa vile niliamini kuwa vile wazungu walinong’a kwa kingereza ” the customer is always right.” Kwa hayo nikapata kununua baiskeli na kupeleka mikate hizi kwa kila lango ya wateja niliopata. Biashara huu ukawa shwari.
Nilitafuta mtuu wa kuwa saidizi wangu wa huu biashara. Kusema kweli kupata mtu mwenye ana uaminifu. Njoroge akawa ananisaidia kuendeleza biashara huu. Mimi na yeye tukawa wanabiashara tukaja pamoja na kupea kampuni letu jina. Jina hilo tukaipea Kate.
Wateja walikuwa kwa wingi na kuendelea kuajiri watu katika kampuni letu la kate. Ilipendezwa mno, na kuanza kutengeneza video kila usiku wa kampuni yao ya kate kuonekana kwa kila televisheni.
Kate ulitumika kila siku na kwa shilingi hamsini tu. Familia nchini uliweza kununua. Serikali ilpendezwa na kaziii hii yetu na kutupa milango yao ya kufanya biashara na wao. Kila sekta ya serikali asubuhu hakuna mikate yalichelewa hata moja.
Sahii namshukuru mola kunipa talanta hii na baraka nimeyapata kutoka kwa jasho langu. Haikuwa rahisi, kwa vile kulikuwa na changamoto hapa na pale. Ndio nawahimiza watoto, kesho inaweza kuwa wewe. Usife moyo. Unaweza kuwa kile unachotaka ukifanya kwa bidii. ” Mzee Azim alihimza na kuendelea ” Mgagaa na upwa hali wali mkaavu.”
Mimi na wenzangu tulisikiliza maneno haya kwa makini. Mzee Azim alimaliza na kusimama. Kando yake alikuwa na mtu wa mkono akimletea simu ya kifahari yani Iphone.
” Ningependa kuendelea watoto wangu lakini nimeitwa kazi. Mungu awabariki.” Natamani kila siku kufikiria kiwango ya hiyo maisha. Niwe na kampuni niwe mfano kama mzee Azim. Tangu hiyo siku, mgagaa na upwa yamenikera akilini mwangu. Hii methali Ilifanya nika fanye kazi kwa bidii.