Insha ya mtaka cha mvunguni sharti ainame

EVERYTHING ON JUMIA


Methali hii inamaanisha kuwa lazima mtu atie bidii ili apate anachotarajia. Methali hii hutumika mtu anpopanga kuwa kitu fulani au kutenda jambo fulani.

Abunwasi alizaliwa katika familia hohehahe maishani mwake aliamua kuwa daktari hospitali kubwa. Wavyele walimpleleka shule. nAlipohitimu darasa la nane alijua kuwa muda unayoyoma na ako tayari kufanya mtihani wa kitaifa katika shule ya msing. Alifuatana na walimu walipoenda kuuliza maswali. Alikuwa na tabia njema shuleni na alitia maanani aliyeambiwa na walimu wake.

Matokeo ya mtihani yalitangazwa. Abunuwasi alikuwa amefaulu na watu walifurahi. Wengi walipenda kusaidia familia yake. Punde, si punde, alipelekwa katika shule ya upili. Hapo alichagua rafiki ambaye alijua atamsaidia maishani. Abunwasi alikuwa anabeba kitabu msalani, wakati wa kula na hadi wakienda kulala. Alijua kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame.

Alipohitimu kidato cha nne, hadi alisahau kuwa mtu anfai kupumzisha akili. Aliendelea kutia bidii za mchwa ajengaye kichunguu kwa mate. Aliwafuata walimu. Wanafunzi wenzake walipokuwa wanatoka nje, yeye alibaki darasani akijisomea. Pia alikuwa anademka dem dem ili kusoma kabla ya wenzake kuamka.

Baada ya wiki si nyingi, matokeo ya kidato cha nne yalitangazwa. Abunuwasi alifurahi kama kibogoyo aliyepata meno wakati wa mlo aliposkia ameongoza nchi nzima. Aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu. Hapo alijihadhari sana na tabia za wenzake. Hakuwa na huusiano na msichana kwa kuwa alijua bado haja fikia umri wa kuoa. Mwishowe alimalizia masomo ya chuo kikuu na kupata kazi nzuri ya kuwa daktari.

Katika harakati zake, alipatana na kipwa mmoja aliyekuwa mrembo. Alikuwa mrembo ungedhani mungu alichukua siku kadhaa za kumuumba. Alikuwa na miguu ya cherehani isiyo na mang’omba wala matege, ilikuwa isiyo kama sanamu iliyofinyangua na kukamilikika bila chembe ya dosari na kwa kweli, alikuwa mrembo kupindukia.

Baada ya muda mfupi, waliamua kuoana. Walifanya arusi kubwa ili wawe mume na mke. Walifurahia walipovishana pete. Baada ya kufunga pingu za maisha, waliamua kuishi maisha mazuri. Walizaa watoto na kuwaelimisha jinsi wao walivyo elimishwa.

Abunwasi aliamua kutoka huku na kuenda kuishi katika marekani na jamii yake. Huko maisha yalikuwa bora kuliko huku. Alinunua gari la kifhari. Hakuwasahau au kuwazika katika kaburi la sahauw wavyele wake. Mara kadhaa walikuwa wanarudi huku nchini na kuwasilimia wavyele wake.

Baada ya miaka kadhaa, Abunwasi alijua kuwa alikuwa ashafaulu katika maisha yake. Kwa kweli, mtaka cha mvunguni, sharti ainame.



Similar Posts