Insha ya mungu hamsahau mja wake.

sijawahi sahau mwaka huo na siku niliyopata kazi nzuri sana huko Marekani. Wazazi wangu walikuwa na furaha mpwitompwito. Ninakumbuka hiyo siku vizuri sana na ilianza nilipomalizia shule ya upili na kuendelea kwenda kufanya masomo ya chuo kikuu niliyokuwa na tarajia.

Lakini wazazi wangu hawakuwa na karo ya kutosha kwa kuenda shule niliyotarajia. Nilishikwa na huzuni sana kwamba machozi yalinitoka nikifikiria vile nitapanga kuwa na maisha mazuri kwa maisha yangu ya kesho. sikutaka kuwa maskini ama maisha yawe mgumu kwangu.

Ilibidi nifanye juu chini nitafute usaidizi kutoka kwamarafiki zangu au familia yetu, kuliza wajomba wangu au wazazi wangu. Nilianza kuliza usaidizi kwa marafiki wangu lakini wote walinitoroka na wajomba wangu hawakutaka kuniona tena.

Niliomba mwenyezi mungu anisaidie niendelee na masomo yangu. Hapo nilianza biashara ya kupika na kuuza mandazi ili nipate peasa kidogo. Nilipowaona marafiki wenzagu wakiendesha magari makubwa, Lo! nilishtuka sana, waliponiona walinickeka ” eti sasa unauza mandazi.”

Kila siku nilikuwa nikiomba mungu anisaidie sana katika maisha nijaribu sana kufaulu. Ulipofika januari miaka elfu mbili kumi na tano, nilipata riziki kuwa dereva wa kuendesha wakubwa wanaofanya kazi na kuwa na kampuni kubwa jijini Nairobi.

Nilikuwa nimeanza kufaidika kidogo kidogo na kutuma pesa kwa wazazi wangu wasaidike. Ilipofika Agosti, kumbe mungu hamsahau mja wake. Nilipewa kazi nzuri sana huko marekani.

Nilienda kwa wazazi wangu kusherekea kwa sababu nilipewa kazi nzuri sana ya kuwa manager wa kampuni fulani Nairobi. Tulikula pilau na soda baridi yaliyokuwa baridi shadidi yaliyokuwa tamu kama asali.

Nilishukuru sana kwa mwenyezi mungu kwa kunipea maisha mema kama hii. Tangu siku hiyo nilijuwa watu wanaonijali sana ni wazazi wangu na wameona kila nimepitia. Walinisaidia kwa kuomba, kunijulia hali na kunieleza mambo ya maisha duniani na kunipa nguvu nisife moyo.

Mimi kila siku nawapigia kujuwa hali ya wazazi wangu. Kutoka siku hiyo niligundua kuwa mungu akifunga nafasi hapa, hufungua kwingine.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts