Insha ya mungu si adhumani.

Sasa nala,namywa na najivisha. Sikuamini kama kaski moja nitakuwa jinsi nilivyo. Nimezaliwa katika aila ya uchochole. Mimi ndimi kifungua mimba wa wavyele wangu Bwana na Bi hamisi. Katika familia yetu tumezaliwa waja kumi na wawili.Nyumba yetu ilikuwa imejengwa kwa udongo tukiwa sote hivyo, tulilala Baba, mama nasi sisi wote nyumbani.

Tulitandika ghunia ili aghalabu tujifunike ngozi ya mbuzi au ng’ombe.Wazazi wangu walikuwa wacha mungu. Walipenda pia msomo lakini hawakuwa na uwezo. Waliamini lai lai mosi uchochole utawaondoka.

kwa hakika Mungu si adhumani, lailai hiyo niliamka kama ilivyo desturi yangu na kwenda kutafuta aghalabun kibarua ilikupata chakula cha kaski hiyo. Nikiwa njiani nilipata waja waliokuwa wakibishana. Nilisimama na kuwauliza chanzo cha ubishi wao. Kwa kuwa walikuwa wamenizidii umri walitoweka na kuelekea njia tofauti.

Ghafla bin vuu gari lilipita likiwa walimegsha kwa kasi mno. Kati ya wale waliokuwa wakibishana alinirejea na kunijulia hali. Tukiwa kwenye mazungumzo huku tukitembea, lile gari lili rudi likiwa limebeba wavyele wangu na wangu na kuni amuru niingie ndani. Bila ya kuharibu wakati nilijitoma ndani.

Gari liliegeshwa kwa mwendo wa kasi mithili ya umeme. Baada ya muda mrefu gari lilisimama na tulipewa mavazi tubadilishe. Mavazi yale yaling’aa kama nyota angani. Bila shaka tulibadili na tuka amuriwa tuingie hotelini tuagize tulichotaka.

Hatimaye tulirudi kwenye gari na safari ikaendelea. Nina yangu alituuliza iwapo tushawahi vaa mavazi kama hayo tena. Baada ya muda mfupi tulifunguliwa lango kuu na kutoka kwa gari hilo. Tulishuka sote huku tumeduwana na kukodoa macho tusijue la kufanya.

Hapo ndipo nilikabidhiwa funguo za jumba la kifahari lililojengwa. Nilimuuliza mbona anipe funguo hapa ndipo alipologa kuwa amerudisha shukran kwa wavyele wangu waliokuwa akiwa malaika wa mwezi moja na kumpeleka kwenye kituo cha polisi.

Na alipojua kuwa hana wazazi na kujua kuwa wavyele wangu ndio waliomwokowa alisema kuwa si vyema kushukuru. Hivyo basi jumba la kifahari tukapata na tukapata kazi kupitia kwa binti huyu aliyeokolewa na wavyele wangu. Hakika tenda wema neneda zako walionena hivyo hawakunoa. Hii ni kwasababu nilifurahi mno kwamba niliweza kupata fanisi huo.

Similar Posts