Insha ya resipe. – Middemb.
Insha ya resipe. – middemb.
Insha ya resipe ni mtungo unaonyesha utaratibu na hatua zinzazofuatwa katika utayarishaji wa mapishi. Mwandishi wa insha hii inahitajika kufuata mwongozo ufuatao.

Mwanafunzi azingatie yafuatayo.
– Kiuandika anwani. – Hii itaonyesha aina ya mapishi au chakula. Mfano: Kuandaa ugali.
– Kuonyesha idadi ya watu wanaandaliwa mapishi hayo.
– Kuonyesha vipimo vya viambata vya upishi vitakavyotumia.
– Kuonyesha jinsi ya kuandaa mapishi hayo na vilevile muda utakaotuimiwa katika kila hatua ya kupika.
– Kuonyesha vyakula viambaa by kuandaliwa pamoja na mapishi uliyotayarisha.
Mfano.
A. Kuandaa matoke kwa watu wanne.
Viambata/Vitakavyohitajika.
Ndizi 10
Chumvi kijiko cha chai 1.
Siagi vijiko vidogo 2.
Maji glasi 2.
Utaratibu.
1. Bambua ndizi huku ukiziweka kwaa maji baridi.
2. kata ndizi hizo vipande vidogo vidogo.
3. Zitie ndizi kwenye sufuria. Tia chumvi kisha utie maji kabla ya kuteka.
4. Funika ndizi hadi ziive ( Maji yasiishe ).
5. Zinapoiva , mwaga maji yake, tia siagi vijiko vidogo mbili na upondeuponde kwa kutumia mwiko.
6. Pondaponda hadi ziwe laini kisha fanyilia mchanaganyiko huu pamoja ili kutoa umbo linaloahitajika, weka bakulini kisha ufunike.
7. Andaa matoke haya mezani pamoja na kitoweo ulichochagua. Chaweza kuwa au waweza kula kwa chai.
B. Kuandaa wali wa watu wawili.
Viambata/Vinavyohitajika.
Mchele glasi 2.
Chumvi kijiko kidogo 1.
Maji glasi 3.
Mafuta ya kupikia vijiko 2.
Utaratibu.
1. Tayarisha mchele kwa kuuchambua kuondoa uchafu.
2. Weka maji kwenye sufuria safi mekoni.
3. Tia chumvi kwenye maji hayo.
4. Yanapochemka, ongeza mafuta ya kupika.
5. Osha mchele ili uwe safi tayari kupikwa.
6. Maji yanapotokota, tia huo mchele ndani kisha ufunike.
7. Acha utokote hadi maji yakaribie kuishia kisha upunguze moto kwenye meko hadi utakapokauka kabisa.
8. Pakua wali huo kwenye sahani na uandae mezani pamoja na kitoweo kilichoteuliwa.
Andika resipe juu ya chakula ukipendacho:
Utaratibu wa kupika mchele.
Viambata.
1 kilo wa mchele.
Maji safi lita moja.
Mafuta funiko moja na nusu.
Chumvi mkono nusu.
Utaratibu.
1. Tia maji kwenye sufuria tia kwenye meko.
2. Eka mafuta na chumvi kwenye maji.
3. Tulia hadi maji yatokote.
4. Maji yakishatokota tia mchele wako ndani, kisha ufunike.
5. Subiri kwa dakika thelathini.
6. Funua funiko kisha uwonje kama hayajaiva ongeza maji.
7. Funika tena kisha usubiri.
8. Funua funiko tena angalia kisha utoe mekoni.
9. Pakuwa kwenye sahani kisha unaweza kula kitoweo, maharagwe au viazi.