Insha ya resipe ya kuandaa matoke kwa watu wanne.
Kuandaa matoke kwa watu wanne.
VIAMBATA.
- Ndizi kumi (10).
- Chumvi kijiko cha chai.
- Siagi kijiko Vidogo (2)
- Maji glasi (2).
Utaratibu.
- Bambua ndizi huku ukiziweka kwenye maji baridi.
- Kata ndizi hizovipande vodogo vidogo.
- Zitie ndizi kwenye sufuria. Tia chumvi kisha utie maji kabla ya kuteleka.
- Funika ndizi hizi hadi ziive (maji yasiishe).
- Zinapoiva, mwaga maji , tia siagi vijiko vidogo na unpondaponda kwa kutumia mwiko.
- Pondaponda hadi ziwe laini kisha finyilia mchanganyiko huu pamoja ili kutoa umbo, weka bakulini kisha ufunike.
- Andaa matoke hayo mezani pamoja na kitoweo uliochagua. Chaweza kuwa cha nyama. Maharagwe, njugu karanga, kuku, samaki au waweza kula kwa chai.
