Insha ya risala

Insha ya risala na maana yake.Risala ni ujumbe au taarifa inayoandikwa na mtu au kundi ili upelekwe kwa mtu fulani kwa lengo la kutoa maoni yao au kuonyesha msimamo wao kuhusu swala fulani.

thoughtful ethnic woman with earphones
Photo by Zen Chung on Pexels.com

Risala inaweza pia tolewa kama hutuba mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la watu.

Muundo wa Risala.

1.    Anwani.

–         Risala mara nyingi huwa na anwani ya mwandishi ambayo hundwa kama anwani ya barua ya kirafiki.

2.    Mada.

–         Mada ya risala hutaja anyetuma na anayetumiwa pamoja na kiini cha risala yenyewe. Mada hutangulizwa kwa neno risala. Kwa Kawaida huandaliwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari.

–         Mfano:

–         RISALA YA RAIA KWA WANACHI WA SUDAN KUSINI KATIKA KUITIMISHA KUPIGA KURA YA MAONI KWA AMANI.

3.    Mtajo.

–         Risala hutangulia kwa kutaja anayeandikwa. Mfano: kwa wanachi wapendwa.

4.    Utangulizi.

–         Mlazo ya risala hutegemea hisia za mwandishi kuhusiana na mada inayorejelewa. Mfano: iwapo mwandishi anaandika risala ya rambirambi anaweza kutanguliza kwa kusema : “ Nina huzuni kupokea habari kuhusu ndugu mpendwa bwana  kisimati kilichotokea tarehe kumi na mbili, mwezi wa pili, mwaka wa elfu mbili kumi na moja kufuatia ajali mbaya ya barabarani.”

5.    Mwili.

–         Sehemu hii hutoa ufafanuzi zaidi kuhusu utangulizi na mada kwa jumla. Huonyesha nia ya kuandikwa kwa risala. Pamoja na mambo mengine yanayohiusiana na risala inayotumiwa.

6.    Hitimisho.

–         Baada ya kutimisha maelezo la mwandishi la mwandishi na sahihi huandikwa.

Sifa za risala.

1.    Kwa kawaida ujumbe huwa maalum na unaweza kuhusiana na mada yoyote. Mfano: heri njema au kutoa rambirambi wakati wa janga.

2.    Ujumbe unaotolewa huonyesha  msimamo na uhusiano kati ya watu ama nje.

3.    Risala hunyesha anayetumia na anayetumiwa.

4.    Wakati mwingine hutumia mtindo wa hotuba hasa pale inaposomwa mbele ya kiongozi au hathira.

5.    Hundikwa katika nafsi ya kwanza umoja a8u wingi k.m mimi au sisi.

6.    Huandikiwa katika wakati uliopo.

Umuhimu wa Risala.

1.    Huonyesha uhusiano mwema na kudumisha amani.

2.    Kujieleza na kuonyesha kujitolea au mwaminifu wa mtu au watu Fulani kwa vingozi.

3.    Kumfanya mwandikiwa kuwa na furaha kwa kua kunao wanaomjali.

Mfano wa risala ya rambirambi.

                                                                               Afisi ya waziri mkuu

                                                                               S.L.P, 11001-00100,

                                                                                Nairobi.

                                                                               22/4/2011.

RISALA YA WAZIRII MKUU KWA BIBI DARAHIMA AMANI KUFUATIA KIFO CHA MUMEWE.

Kwa bibi Amani,

Nina huzuni kuu kuipokea habari kuhusu kifo cha ghafla cha mumeo, waziri wa mazingira, bwana heri amani, kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea huko salgaa. Bwana heri alikuwa mtu wa watu. Alikuwa mkarimu na mwenuye kupenda amani na maendeleo. Alijitolea kutekeleza majukumu yaka kama waziri wa mazingira kwa uaminifu yake kama waziri wa mazingira kwa uaminifu mfano, kwenda kwake ni pigo kubwa kwangu, kwa familia na taifa zima kwa jumla.

Ninaweza tu kukisia hali ngumu na uchungu unaohisi wakati huu wa majonzi. Najua kuna mwanga mkubwa niliokwachia wa kuendelea na malezi ya watoto, ila naomba uwe na subira na utayakashinds majaribu yote.

Ningependa kukuhakikishia kama waziri mkuu, kwamba tutazidi kuwa pamoja nanyi wakati huu wa majonzi. Naomba mungu akupe wewe pamoja na familia yenu stahamala wakati huu wa maombelezi.

Wale walioishi katika mioyo ya watu, kama alivyoishi, Bwana heri, kamwe hawafi, Tutazidi kuwaombea wakati wote.

Wako mwaminifu,

Skikomale

Shantum kikomale.

Waziri mkuu.

Mfano wa risala ya heri njema.

                                                                                     S.L.P 300-30,

                                                                                      Torit,

                                                                                     Sudan.

RISALA YA RAIA KWA WANACHI WA SUDAN KUSINI KATIKA KUITIMISHA KUPIGA KURA YA MAONI KWA AMANI.

Kwa wananchi wenzangu,

Nachukua fursa hii adimu kuwapongeza enyi raia wa nchi mpya ya sudan kusini kwa kupiga kura ya maoni kwa amani. Huu ni mwamko mpya katika bara letu la afrika na 

dunia

 kwa jumla.

Kwa muda mrefu, tumeteseka na vita vya kikabila. Vita vilivyosababisha umwagikaji mwingi bwa damu. 

Raia wengi wasio na hatia waliangamia . Ndugu na jamaa nao 

walitenganishwa kikatili. Mayatima wakaongezeka  watu wengi walisononeka 

kutokana 

na majeraha waliyopata vitani. 

Kambi za wakimbizi zikaenea kote. Wakimbizi waliishi maisha 

yaliyojaa mateso, dhiki na ukiwa kwa

 zaidi ya miaka ishirini na moja. Miongoni mwa kambi zilizojaa

 maelfu ya wakimbizi ni ile ya kakuma iliyo katika sehemu kame nchini kenya.

Siku ya leo, raia wapendwa, hayo yote mmeyaweka katika 

kaburi la sahau. Mmepiga kura zenu kwa

 amani na 

utulivi na kujipa uhuru. Tuna matumaini kuwa azma ya wanachi katika nchi mpya 

itaafikiwa, na kwamba matarajio ya 

mamilioni ya watiu yatatimizwa. Rasilimali za nchi hiil, 

zikiwema utajiri mkubwa wa mafuta. 

Zitalindwa na kutumiwa kwa manufaa ya raia wote ili nchi 

yetu istawi.

Raia wapendwa. Nchi hii pia itahitaji kusaidika na jamii ya 

kimataifa ili uwezo hukua. Miundo –msingi kama vile barabara, shule za msingi na za upili, 

Vyoo vikuu na hospitali ni sharti zijengwe. Sekta za kilimi na biashara sharti zimarishwe ili raia waweza 

kupata chakula kwa bei rahisi na 

kwa wingi. Jamii yenye afya njema hufanya kazi tufikie 

malengo haya. Ningependa kuomba jamii ya 

kimataifa itusaidie katika kujiendeleza kisiasa, kiuchumi 

kijamii na kiidini maana hii ndiyo

 itakayokuwa nchi changa zaidi barani Afrika na ulimwenguni.

Raia wapendwa, nawatakia heri na ufanisi wakati huu 

tukisubiri kupiga hatua  nyingine mbele 

ya kujenga taifa letu. Asanteni sana na mungu awabariki.

Ni mimi

Bwana Mwahaki.

Raia wa sudan.

HITIMSHO: Mwisho huonyesha msimamo wa mwenye kutuma 

visala, uzalendo, shuleni, Majonzi , 

kutegemea mada ya risala.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts