Insha ya safari ya Ajabu.

Nilianza safari yangu kabla ya Jua kupasua wingu. Nilikuwa nimeshafunga virago vysngu vyote na nikatoka mastakimuni mwangu Kwa makini Kwani sikusahau kuwa malenga mmoja alinena mbio za sakafuni hushia ukingoni.

Hii ilikuwa safari niliyogopa kufanya katika maisha yangu yote. Safari hii haikuwa ya kawaida la hasha! Ilikuwa safari ya kulitatua zimwi lilomea firisha babu yangu Hali jongomeo bila nauli.

Kuikuwa na baridi Kali mno kwani jua lilikuwa Bado halijachomoza katika safari yangu,niligawa na mawazo ya woga wa kila aina. Niliyogopa sana Hadi nikasimama wima na kutaka kurudi nyumbani. Nilipokumbuka ya kuwa Kwa mwoga huenda kicheko, niliendelea na safari yangu kiba kibandika kiba kibandika Kwa mwendo wa lumbwi.

Jua lilipojitokeza, nilikaa chini kitako na kustaftahi Kwa dakika chache TU baada ya kuchukua kiamsha kinywa. Nilitoa ramani niliochotewa na mhaguzi gwiji wa Kijiji chetu. Niliichunguza Kwa makini kabla ya kuikunja na kuitua mkobani.

Safari yangu ilichukua siku thenashara kamili ilijawa na matatizo chungu nzima na nilijawa na simanzi isiyo na kifani. Hata hivyo , sikukata tamaa wala kugota. Mara Kwa mara nilitolewa shoti na wanyama wa porini lakini Kwasababu nilikuwa nimekonda kama ng’onda nilikuwa na mbio za umeme.

Nilipofika kwenye Kijiji Cha maji ya kila aina, roho yangu iligwanyika mara mbili na kuluimbikia magotini. Niliona haya ya kumlilia mamangu lakini nilijikaza kisabuni.

Kijiji hicho lilikuwa kizuri mno Baraste ilikuwa ya dhahabu ilingara mno na Mili ya zamburau ilitoa Almasi yenye thamani isiyoelezeka. Hii ilionekana kama nchi ya maziwa na uki. Nchi iliyojua Raha na buraha na buraha. Nilishangazwa sana.

Vitu vilivyoadimika kama barafu ya kukaanga huko kwetu vilikuwa vimejaa tele Nilipokuwa nikizuru nchi hiyo nzuri, jini moja lilitokea mbele yangu.

Lo! Niligutuka sana lakini lile jini lilicheka kwa nguvu Hadi nikafedheka. Kufimba na kufumbua,lilinyamaza kimya na kuniongelesha Kwa dharau. ” Kwa Nini unanitaka?. ” Nilipigwa butwaa chakari Kwa jini lile ulinyua kama kiganja Cha mkono wake.

” Usiogope” lilisema, “Nitakuambia sababu ya kumuua babu yako.” Roho yangu ulidunda Kwa nguvu na barasa na hamsa kama ngoma za hanzua. Hapo ndipo lile jini lilinibeba juu Kwa juu huku nikiyugayuga kama tumbili alingepoteza mwanawe mtini.

Punde si punde, nilijikuta mbele ya babu yangu. Nilijaribu kumwita lakini alionekana kama mtu aliyetia maskio nta na aliyekataa kusikia la mwadhini. “Usijichoshe Bure.” Jini yule liliniambia. “Hawezi kukuskia. Tumerudi miaka kumi iliyopita ili ujionee matendo ya babu yako!.”Ama kweli wahenga na waligonga ndipo walipokuwa chini kitako wakidondoa mchele waliposema ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni.

Lahaula! Nilimwona babu yangu akiongoza genge la wezi na kuvamia Kijiji Chake mwenyewe. Watu wengi walipoteza maisha Yao lakini hakuna hata mmoja aliyeshuku babu. Majasusi waliitwa lakini wote waliambulia patupu kwa kweli kikulacho ki nguoni mwako.

” kazi yetu ni ya usalama.” Jini lilinieleza “Babu yako alikuwa mwizi na alisahau kuwa siku za mwizi ni arubaini. Usimweleze mtu Yale uneyaona ama sivyo tutachukua maisha yako pia.”

Jini Hilo liliponieleza hayo, lilipotea Nami nikajikuta nyumbani. Sikuamini Yale niliyoyagundua lakini nilinyamaza kimya na kutulia tuli laiti ningaligundua tabia ya Siri ya babu kabla Aage Dunia. Ningalimwelezea kuwa kumla nguru si kazi, kazi kumwosha.

BLACK FRIDAY DEFACTO DEALS

Similar Posts