Insha ya shajara

Insha ya Shajara maana na sifa zake.Shajara ni rekodi ya mambo muhimu yanayotokea  kila siku. Shajara inaweza kuwa rasmi au ya kibinafsi. Shajara huandikwa katika kitabu maalum ambacho huwa na nafasi ya kujaza mabao ya kila siku.

–         Mambo yote muhimu yaliyotokea au yanahitaji kukumbukwa huweza kuandikwa ndani ya kitabu ya kila siku.

–         Pia mambo yanayokusaidia kufanya muda ujao huandikwa.

Muundo wa shajara.

1.    Shajara huwa na kichwa m.f kama ni shajara ya kibinafsi unaweza kuandika, “ shajara ya kibinafsi.”

2.    Baada ya kichwa huwa ni siku na tarehe ambapo mambo tofauti yalifanyika.

–         Tunaweza andika kile kilichotakia au kinachonuiwa kufanywa kwa siku hiyo.

Sifa za shajara.

1.    Shajara hundikwa kwa ufupi.

2.    Huandikwa kwa wakati uliopita isipokuwa unapoandika jambo ambalo unanuia kufanya katika muda ujao.

3.    Shajara za kibinafsi huwa ni siri za mwenye kuiandika.

Umuhimu wa shajara.

1.    Shajara huweka kumbukumbu ya matukio ya kibinafsi au ya kiofisi.

2.    Shajara huhifadhi taarifa muhimu pamoja na siri za mtu binafsi au za shirika fulani.

3.    Huwezesha mtu au shirika kupanga vyema mambo yake iwapo inatumia kurekodi mambo yatakayo fanyika.

Similar Posts