Insha ya sheng.
Ilikuwa sato, ambapo niliamka asubuhi kupata Mkoro wangu alishakuwa ameenda kazi. Kwa meza niliachiwa doe ninunue oredho kwa duka. Nilienda polepole kwa duka nikabuy, nikarudi kejani ktulia tu nikiwatch movie fulani ya dj afro.

Kufika hivi mid day hapo niliskia kuan text kwa tenje yangu. Kuicheki text ilitoka kwa morio wangu anaitwa brayo. Brayo ni bro mine wa nguvu na nimemcheki na amenicheki vilke tume grow. Akanishow “rada si ukam kwangu hivi, najua umeboeka.” Enyewe kuna vile niliboeka na atleast ni poa ujimbambe na beshte yako.
Nilivaa ndula zangu kuendea kuelekea kwa kina brayo. Kufika niliona ni kama brayo alikuwa na bash juu niliona wasee walikuwa wengi, mayengs na kidogo kidogo kuingia ndani hivi kutafuta brayo. Nilimcheki nikamuuliza “ala kwani nini ina happen?.” akanijibu ” Bro kwani huoni leo ni sherehe, cheki fanya hivi jibambe.”
Nikamwabia ” we uko aje si ungenishow ni sherehe sa cheki vile nimevaa.” Brayo akanishow ” cheki enda uchange tukona trip hadi naivasha na uchangamke bro.” Mimi nani nilikimbia mbio hadi kejani kuchange. Nikaosha uso hivi hivi nikjispray perfume nikajua leo leo.
Kutoka kejani sikuwa na haraka, nilitembea mos mos nikielekea kwa kina brayo. Kufika huko ala wase wameenda wapi. Nikachukua tenje yangu kumcall. ” hello, ala kwani uko.” brayo kajibu ” kwani hauko ndani ya gari.” mimi nikamjibu zii. ” aaah pole bro iza si tushatoka kuelekea.” kusikia hivo nilizima simu nikaenda home kama nimeudhika enyewe brayo hakunidoo fiti.
