Insha ya tahadhari – maana yake na sifa zake.

Insha ya tahadhari – maana yake na sifa zake.Tahadhari ni maelezo yanaoyotolewa ili kufahamisha kuhusu kutokea kwa hali fulani. Hutolewa kueleza hadhari za mbali husika hasa panapokuwa na hatari ya madhara.

Sifa za tahadhari.

1.   Huwa na anwani, tarehe ya kuandikwa.

2.   Huwa na lengo ya kuandika kwake.

3.   Jina la mwandishi na cheo chake.

4.   Huwa na sahihi ya mwandishi.

–        Kuna aina mbili za tahadhari.

1.   Ilani.

2.   Onyo.

Ilani – ni aina ya tangazo ambalo hutahadharisha kuhusu aina ya jambo au tukio ambalo inastahili kuepuka la sivyo madhara yatokea.

Mfano.

POMBE ISIUZWE WATU WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 18.

WIZARA YA AFYA ,KUPITIA KWA HOSPITALI YA KAUTI. INAWATANGAZIA KUZUKA KWA UGONJWA HATARI WA KIPINDUPINDU. WATU WOTE WANASHAURIWA KUZINGATIA USAFI WA MWILI NA MAZINGIRA. ILI KUKINGA KUTOKANA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUU. MAMBO YAFUATAYO NI SHARTI ITUMIWE.

1.   KILA MTU AHAKIKISHE ANATUMIA CHOO.

2.   KILA MTU ANAWE MKONO KWA MAJI SAFI  NAS SABUNI BAADA YA KUTOKA MSALANI.

3.   HAKIKISHA UNAKULA MAHALI PA SAFI, WATU WASIWE KWENYE MKAHAWA.

4.   MTU MWENYE DALILI ZA KUENDESHA NA KUTAPIKA AKIMBIZWE HOSPITALINI KWA UCHUNGUZI MAALUM.

5.   ALIYE AMBUKIZWA APEWE MAJI YA MENGI YA KUNYWA WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALINI.

6.   KILA MTU ACHEMSHE MAJI YA KUNYWA.

7.   MTU YEYOTE ALIYEAMBUKIZWA ATENGWE NA WATU WENGINE NA ATAFUTIWE MATIBABU YA HARAKA.

MUHIMU: MTU YEYOTE ATAKAYEPATIKANA AKIUZA CHAKULA KATIKA MAENEO WAZI ATASHTAKIWA.

–        onyo huandikwa kuonya mtu dhidi ya kufanya jambo fulani.

–        Onyo ina sifa sawa na ilani.

Similar Posts