Isimu jamii – na umuhimu zake na maana
Isimu jamii na umuhimu zake na maana. Isimu jamii – ni matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. ( Jamii ) kama vile; sokoni, mahakamani, hospitals, shule, michezo, kwenye utafiti, hotelini, biashara n.k.
– Lugha huitwa sajili pia

Sajili ya lugha hutegemea mambo yafuatayo.
– Wahusika – msamiati hulebga wahusika yaani watumizi wa lugha.
– Uhusiano wao – kama ni kirafiki, kikazi , kihadhi au cheo.
– Mahali – mazingira yanaweza kuwa tulivu, furaha, huzuni , fujo.
– Tukio lenyewe – lugha hutegemea matokeo kama vile: mkulima, kucheza, matokeo, harusi.
– Umri – sajili yeyote hutegemea.
– Tabaka – lugha yeyote hutegemea cheo kama ni tajiri au maskini.
– Jinsia – hali ya kuwa mwanamke au mwanaume kwa wanawake kwa wanawake wana lugha yao.
– Elimu – sajili hutegemea kiwango cha elimu.
– Wakati – msamiati hubadilika kutegemea wakati m.f msamiati wa teknolojia mpya. Kwa vile rununu, televisheni, wafuti, kipepesi, mtandao wa kijamii wakati huu.
