Insha ya mbovu harabu ya nzima.

EVERYTHING ON JUMIA

Methali hii inatuonya kuwa haifai kuandama na watu wenye tabia mbovu kwani huenda wakatuambukiza uovu wao na kuharibu tabia zetu nzuri.Hapo zamani za kale paliishi kijana mmoja aliyeitwa majivuno. Aiishi katika kijiji cha songambele. Alikuwa na tabia ambazo hazikuwapendeza wanakijiji.
Alipelekwa shuleni angalau asome lakini wapi? Wavyele wake walijaribu kumwambia mtoto wao lakini hakuambi, licha wala hakusemezeka.Aliwapotosha vijna wengi wa kijiji cha songa mbele. Alizitumia dawa za kulevya kama pombe. Wazazi wa vijana wa kijiji walilalamika majivuno apelekwe kituoni mwa polisi.
Majivuno alikuwa mtu mwenye maneno mengi kama kasuku. Aliwatuoia maneno watu waliomzidi umri hapo kijijini. Walimu shuleni walimwadhibu lakini wapi?. Aliwatishia pia walimu wake shuleni. Lakini wahenga hawakukosea waliposema asiyeskia la mku huvunjika guu.Majivuno hakukosa watu wakuandamana naye huko kijijini songambele, vijana wengi walikuwa wamepotoshwa na majivuno, walijaribu kujitengana naye lakini muda ulikuwa umeyoyoma.Siku moja walipanga kuiba katika duka fulani sokoni. Walivunja milango na kuiba pesa. Lakini wahenga hawakukosea waliposema siku za mwizi ni arobaini. Baada ya wiki moja, walijulikana walifungwa katika chuo cha polisi.Maisha yao yalikuwa hatarini. Walifungwa kifungo cha miaka yote hadi wakaage dunia. Kweli walijua walikuwa wamejiharibia maisha yao ya baadae naam. Majuto ni mjukuu huja baadaye.

Similar Posts