sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma insha.
Kwa maneno ya Mama imeninginia akilini mwangu kila siku nikiwa gerezani pamoja na wenzangu. ” Mtego wa panya huwanasa waliomo na wasiokuwamo.” kila mtu ana hadithi zake hapa na mbona waeshtakiwa kwa mashtaka kwa wengi usiofaa.

Lakini kwa kosa langu ndio ni mimi nimekubali. Na mashtaka yangu ndio naipita, kwa kweli moyo wangu unahisi uchungu mno kwa jambo nilichofanya nikiwa mwanafunzi shuleni ya upili. Ningaliskia, nisingalikuwa papa hapa kuitwa kila saa mfungwa nane tisa kumi.
Maneno haya hainifurahishi mno. Ndio nina hadithi yangu na vile nililipata papa hapa gerezani kwa wenzangu kuna wale walitolewa kwa pesa na kwa njia za ufisadi. Wengine wazazi wao wako ndani ya sekta wa serikali ambapo walioachiliwa. Lakini mimi ndio mkono mrefu wa serkali ulinipata, na si vichekesho.
Nilikuwa mwanafunzi kutajika. nilikuwa na sif maridhawa. Mambo kuhusu kesi au kusumbua walimu haikuwa ikisikika kutoka kwangu.. Nilipenda kila mtu ikiwa mzazi, mwanafunzi, walimu wote niliwapenda bila ya kuzingatia mwemas wala mui.
punde si punde, nilijipata kwa shida nilisolielewa kwa kuwa marafiki wa chanda na petewakawa wamebadilika. Na hapa ndipo nilijipata katika shimo lisilo na mwisho ila mwishowe ulikuwa giza nene, singeweza kutoka humo.
tukiwa likizo nilikaribishwa na marafiki zangu katika sherehe nisiyoelewa lakini nilialishwa kuwa ni kusherekea kuzaliwa kwake. Nilipatana na wenzangu na vitu vilivyonunuliwa yalikuwa vya mshangao lakini kwangu hukunishtua..
Pombe, sigara na dawa zute za kulevya ilisemekana ulikuwa kawaida kwetu. Sherehe huu kila mtu alikuwa sawa kivyake. Wengine wanakutana wakiwa wawili wawili. Hapa mmoja ana mpenzi wake. Ikiwa msichana, amemweka mvulana, ikiwa mvulana ameweka msichana. Wanatembea kwa sako kwa bako wakizumgumz. Utamu wa mapenzi ati.
KIla mtu ana raha mustarehe kama sultan bin jerehe. Lakini nisilolijua, ndio nilikuja kugundika baadaye. Jua likashatua magharibi na giza kugubiza mandhari ya nyumbani humu. Giza ukaingia totoro na na baridi ukaanza kuihisi ni shadidi.
Nje kulikuwa na sauti mkubwa isiyoeleweka ” haja sherehe umeisha na nataka kila moja atoke polepole.” kuenda kuangalia dirishani, niliona mataa za magari hapa tukizungukwa kama mviringo. Kwa vile niliyoitambua , ilikuwa karadinga, na polisi walikuwa njee kutungoja wakiwa wameshika bastola. Lakini je ni makosa gani tumefanya?.
Ghafla bin vuu tuliskia mlio wa bunduki na sisi sote tukawa tumelala chini kama nyau. Kidogo kidogo tulitoka moja moja na kuchunguzwa maskari hawa. Wenzangu walipatikana kuwa wezi. Na mimi nikashukiwa kuwa moja wao.
kortini nilipitia , na kufungwa kwa mashtaka wa miaka mitano gerezani na hawa majangili wanojiita wenzangu. Nikavuliwa madarka yangu niliyokuwa nikitamba nayo.
Ndio wenzangu waliachiliwa, lakini wazazi wangu hawana mali, hawana pesa, hawako katika sekata wa serikali au magari za kifahari. Kwa mashtaka niliyopewa…….. sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Kwangu kwa wale hawana haki.
