Sifa za misimu na umuhimu sake.

Misimu Ni maneno au semi zinazo zuka katika jamii na kutumiwa na watu ambao huelewana. Hutumiwa kama siri miongoni mwao kwa kuwa wanaelewa maana ya maneno au semi hizo.



Mifano ya misimu.

– sonko – tajiri.

– Kuasha mataa- kulewa pombe.

– Piga ngeta – kumwibia mtu kwa kupinzia na kumkaba.



Uundaji wa misimu.

– Hupitia utohozi wa misimu. K.m windo, dirisha, Gava ( Government), Dereva ( Dere).

– Hupitia sitiari kwa mfano: Nyani – goalkeeper, Kasuku – mtu anayependa kungea sana, nyoka – adui, fisi – mlafi.

– Hubadilisha maana ya kawaida ya maneno. Kwa mfano: chuma – gari ya kifahari, Toboa – kufaulu, Mguu wa bata – bastola.

– Uhunguzi wa maneno mapya. Km zii! – Hapana ama kukataa.

– Kuchanganya lugha. K.m Kubeaf, kurelax, kujiwaste.



Sifa za misimu.

– Hubuniwa na kutoweka baada ya muda. K.m Manyanga – upya.

– Baadhi hubadilika na kuwa lugha k.m Toa chai – honga au hongo.

– Bodaboda – pikipiki.

– Hujikita katika vikundi mbalimbali ya wanajamii mfano misimu ya vijana, wazee na wazazi.

– Hutumia lugha ya kimafumbo k.m machozi ya simba – pombe kali sana.



Misimu huwa na maana tofauti tofauti.



– Ni kigezo mojawapo cha kuwashiria mabadiliko katika historia cha lugha fulani.

– Matumizi ya misimu hutegemea sababu za kuitumia, tabia za watumizi, mada husika jinsia, umri wa wahusika mazingira ya utumizi.

Umuhimu wa misimu.

– Hutumiwa ili kufucha siri.

– Ni njia ya kujitambulisha nyakundi fulani ya watu.

– Huficha lugha chafu au matusi kwa mfano; naenda kuua nyoka – msalani.

– Hutumika kufidhia kuongelea ukosefu wa samiati.

– Hutumiwa kuhaisisha mawasiliano miongoni wa wanajamii.

– Hutumiwa kuashiria haba ya lugha katika vipindi mbalimabali ya kihistoria.



Similar Posts