10 Sifa za nyimbo na umuhimu wake


Nyimbo ni maneno yaliyopangwa kumuziki. Kuna kupanda na kushuka sauti katika mapigo.
Sifa za nyimbo.
– Hupanda na kushuka kwa sauti.
– Hutumia lugha ya mkato.
– Inapangilio wasilabi mishororo wa ubeti.
– Ina mapigo ya kimziki.
– Utumiaji wa lugha mzito inayoibua taswira na hisia kama za mapenzi, huzuni na furaha.
– Huandamana na ala za muziki k.m; ngoma, baragumu, msewe, zumari.
– Hufungamana na miktadha mbalimbali kama vile; kazi, haru, juando na nyando.
– Badhii ya vifungu hurudirudiwa – kibwagizo, kitikio au mikarara.
– Huandamana na uchezaji wa viuongo kama vile mabega, kupiga makofi, na mipigo la miguu.
Umuhimu wa nyimbo.
– Hutambulisha jamii k.m ukulima uvuvi n.k.
– Hutoa hisia za moyo.
– Ni njia ya kuhifadhi utamaduni na historia ya jamii.
– Hutunguiza.
– Hupitisha amali au mawaidha.
– Hukuza ubunifu.
– Ni njia kupatia riziki.
– Ni njia ya kukuza talanta.
Aina za nyimbo.
1. Mbolezi – huimbwa katika kati ya kumboleza au matanga.
2. Nyimbo za dini – katika ibada.
3. Nyimbo za vita – husisitiza ushujaa na uzalendo.
4. Mawimbo za mapenzi – huimbika na mpenzi, ulimbwende au usaliti.
5. Bembelezi – huimbiwa kwa watoto kuwafariji au kumbembeleza walale ama waache kulia.