Vitendawili sifa na aina zake.

Vitendawili ni fungu la maneno linalo na maana fiche mtu hutajika kufikiria ili maana kufumbuliwa.
Sifa za vitendawili.
– Huwa na formular maalum.(mtindo wa kwanza) – Kitendawili ………. tega.
– Husisha vifungu vinachohitaji kufunguliwa.
– Anayetegua anaposhindwa anatoa zawadi ama jibu.
– Hurejelea mambo ya kawaida katika maisha na mazingira ya wanajamii.
– Aghalabu kitendawili huwa na jibu moja tu.
– Hutumia lugha ya mkato – kauli au sentensi moja tu.
– Huchemsha bongo
– Huelimisha wanajamii.
– Hukuza stadi ya umakinifu.
– Huburudisha hadhira.
– Hukuza ufasaha wa lugha.
– Ni njia kuhifadhi utamaduni na historia ya jamii.
Aina za vitendawili.
– Vitendawili sahili (kawaida).
– Vitendawili changamano.
– Vitendawili vya sauti.
– Vitendawili mkufu.
1. Vitendawili sahili – kwa mfano: chakula kikuu cha mtoto – maziwa.
2. Vitendawili changamano – kwa mfano: amezaliwa ali, amekufa hali, amerudi hali – Nywele.
3. Vitendawili vya sauti – Chubuluu! – linapoanguka majini.
4. Vitendawili mkufu.(virefu) – Asubuhi ana miguu minne, saa saba ana miguu miwili, na jioni ana miguu mitatu. : Mtu akiwa mtoto, umri wa makamuu na akiwa mzee.
